NA. MWANDISHI WETU -NKASI

Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu imewajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Wataalamu ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa ili kuhakikisha jamii inakuwa stahimilivu wakati wa majanga.

Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 19 Januari, 2026 na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa kikao cha kupitia Rasimu za Nyaraka za Usimamizi wa Maafa za Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa wilayani humu ikiongozwa na  na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.

Kikao hicho kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kikilenga kuwapitisha katika nyaraka zilizoandaliwa kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri ambazo ni Tathmini ya Vihatarishi vya Majanga, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Majanga, Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa pamoja na Mkakati wa kupunguza vihatarishi vya maafa.

Akitoa neno la shukran mara baada ya kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Bw. Eliud Njogellah amepongeza kazi iliyofanyika na timu ya kuandaa nyaraka hizo huku akieleza kuwa zimekuja kwa wakati sahihi ambapo Halmashauri imekuwa ikikumbwa na majanga na maafa mbalimbali hivyo zitatumika kwa uzito wake na tija iliyokusudiwa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...