Mamlaka ya uwekezaji inayosimamia maeneo maalumu ya kiuchumi TISEZA imezindua ziara yake mkoani Geita ikiwa ni mwanzo wa Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani yani utekelezaji kwa vitendo wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Miaka Mitano.

Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA balozi Dr Aziz Mlima amesema kuwa Kampeni hii inalenga kubadili fikra na mtazamo uliopo miongoni mwa Watanzania kwamba Uwekezaji ni mahususi kwa Raia wa Kigeni na sio kwa Watanzania kwa kutoa Elimu ya Uwekezaji kwa makundi mbalimbali katika jamii na kujenga hamasa itakayosaidia kuchochea mwamko na kuongeza idadi ya wawekezaji wa Ndani.

Bodi ya TISEZA ikiwa mkoani Geita imefanikiwa kutembelea wawekezaji ambao ni miongoni mwa wawekezaji ambao wanauingizia mkoa wa Geita fedha kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na ziara hiyo ya kukagua miradi ya wawekezaji mamlaka imedhamiria Kuendesha semina na Makongamano ya Uwekezaji kwa makundi mbalimbali katika jamii yanayojumuisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SMEs), wafanyabiashara, Vijana, wanahabari, Maafisa wanaosimamia viwanda, Biashara na Uwekezaji katika Sekretariet za Mikoa na Halmashauri, na Wawekezaji

Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela amepongeza mamlaka ya TISEZA kwa kufanya ziara hiyo mkoani Geita kwani itawawezesha wawekezaji mkoani humo kujifunza na kujua haki na Sheria kupitia mamlaka hiyo.

"Kama mkoa tunafanya jitihada za kuhakikisha fursa za kiuchumi zinatambulika na kuhakikisha hakuna sekta ya kiuchumi ambayo itakuwa imelala "alisema Shigela

Mamlaka hiyo ilisajili jumla ya miradi 901 Yenye thamani ya bilioni 9.31 kwa mwaka 2024, na Sasa imefanikiwa kusajiri miradi 927 kwa mwaka 2025 yenye thamani ya bilioni 11.ambapo jumla ya miradi 469 inamilikiwa na watanzania sawa na asilimia 51%.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...