Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda ameipongeza taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kuendeleza juhudi za kusaidia watoto wa familia zenye uhitaji kwa kugawa sare na vifaa vya shule, akisema hatua hiyo inaunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha elimu jumuishi na bora kwa wote.
Mkenda ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kugawa sare na vifaa vya shule kwa watoto 400 kutoka vituo saba vya makao ya watoto jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na taasisi ya LALJI FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya taasisi hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali kuinua elimu kwa watoto kutoka familia zenye uhitaji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkenda amesema hatua hiyo ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu inaonyesha mshikamano wa taasisi binafsi na Serikali katika kuhakikisha elimu inapatikana kwa usawa na bila ubaguzi.
“Watoto hawa sasa watajiunga na wenzao mashuleni wakiwa na furaha na hali ya kujiamini Watakuwa na sare, mabegi, viatu na vifaa vya kujifunzia sawa na wenzao. Hii ni hatua muhimu katika kuondoa unyonge na kuleta matumaini mapya kwa watoto hawa,” alisema Prof. Mkenda.
Kwa upande wake, Kamishna wa Elimu Tanzania Lyabwene Mutahabwa alisema msaada huo utapunguza changamoto zinazowakabili watoto katika kuanza mwaka wa masomo.
“Watoto hawa sasa watahudhuria shuleni kwa wakati, bila kubeba mzigo wa kutafuta sare au vifaa. Hii itaongeza mahudhurio na hatimaye kuongeza ufaulu,” alisema Mutahabwa.
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir, aliwahimiza Watanzania kutenda matendo ya huruma kwa jamii, hasa kusaidia familia zenye uhitaji.
“Kutoa kwa ajili ya wenye uhitaji ni ibada inayompendeza Mwenyezi Mungu. Wito wangu kwa jamii ni kujitoa kusaidia kadiri ya uwezo wetu, kwani thawabu ni kubwa mbele za Mungu,” alisema Mufti Zubeir.
Kwa upande wake mlezi wa taasisi ya LALJI FOUNDATION Mohsin LALJI ( Sheni) alieleza kuwa taasisi hiyo itaendelea kusaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii, ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...