Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili, huku akisisitiza kuwa mkakati huo ni nguzo muhimu ya ujenzi wa taifa linaloongozwa na maarifa, sayansi na teknolojia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema mpango huo ni miongoni mwa ahadi za siku 100 alizozitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, na kwamba unalenga kuimarisha msingi wa elimu kwa watoto ili waweze kukabiliana na masomo yao kwa ufanisi kadri wanavyopanda ngazi za elimu.
“Kama hatutaweka msingi imara wa elimu kwa watoto wetu, tutajikuta tunajenga juu ya msingi dhaifu. Ndiyo maana mkakati huu ni muhimu sana kwa mustakabali wa elimu, uchumi na maendeleo ya taifa letu,” amesema Dkt Samia.
Amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Sera ya Elimu na Mafunzo pamoja ya mwaka 2014 na kutekeleza ajenda za kikanda na kimataifa ikiwemo Azimio la Umoja wa Afrika kuhusu elimu ya Afrika na lengo Namba nne la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) linalosisitiza elimu bora na jumuishi.
Aidha amesisitiza kuwa serikali imejizatiti kuhakikisha hakuna mtoto atakayefika darasa la tatu bila kumudu stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu, ikiwemo watoto wenye mahitaji maalum, kwa kutumia mbinu rafiki za ufundishaji zinazozingatia vitendo na mazingira halisi ya mtoto.
Katika hatua nyingine, Rais Samia aliipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuhamasisha matumizi ya zana za kufundishia zinazotengenezwa kwa malighafi za ndani, akisema ubunifu huo unasaidia watoto kuelewa kwa vitendo masomo ya kusoma, kuandika na hisabati.
“Nimeona teknolojia bunifu zilizotengenezwa na wabunifu wetu hapa hapa nchini kutoka kwenye vifaa vya mbao, chupa, mchanga hadi vifaa rahisi vinavyomshirikisha mtoto moja kwa moja katika kujifunza,”
Ameongeza kuwa mafanikio ya serikali katika kuimarisha miundombinu ya elimu, akibainisha kuwa kati ya mwaka 2021 hadi 2025, serikali imejenga takribani madarasa 34,000 ya shule za msingi na zaidi ya madarasa 9,000 kila mwaka ya sekondari, sambamba na kuajiri walimu zaidi ya 7,000 ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunzia
Aidha amesema, watahakikisha Walimu wanakuwa sehemu ya suluhisho na wadau muhimu katika utekelezaji na kupewa nyenzo na mbinu za kisasa za ufundishaji zote zinazotakiwa.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Said Mohamed, alisema uzinduzi wa mpango huo ni hatua ya kihistoria na ya kimapinduzi katika sekta ya elimu, akisisitiza kuwa umahiri wa KKK ndio msingi wa mafanikio ya elimu katika ngazi zote.
Alieleza kuwa tathmini za kitaifa za KKK zilizofanywa kuanzia mwaka 2015 hadi 2023 zimeonyesha kupungua kwa idadi ya wanafunzi wasiokuwa na umahiri wa stadi hizo, jambo linaloashiria mafanikio ya jitihada za serikali katika kuboresha elimu ya msingi.
Awali Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema uzinduzi wa mpango huo ni utekelezaji wa moja kwa moja wa maelekezo ya Rais Samia, akibainisha kuwa wizara hiyo itaendelea kuimarisha mafunzo kwa walimu, upatikanaji wa vifaa vya kufundishia, tathmini za mara kwa mara na ushirikishwaji wa wazazi na jamii kwa ujumla.
“Mpango huu ni wa miaka mitano na tutahakikisha utekelezaji wake unasimamiwa kikamilifu ili matokeo yaonekane moja kwa moja kwa mtoto wa Kitanzania,” amesem Prof. Mkenda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...