Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha.

Msaada wa kisheria wa Samia Legal Aids umeahidi kurudisha tabasamu kwa wananchi kwa kuwapatia msaada wa kisheria katika migogoro inayowakumba hadi pale ufumbuzi unapopatikana.

Akizungumza katika mkutano wa wanasheria kutoka sekretarieti za mikoa wanaotoa msaada wa kisheria kutoka  SAMIA LEGAL AIDS nchi nzima, Mkurugenzi wa sheria ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Wakili Richard Odongo amesisitiza kuwa lengo kuu ni  kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa kupata huduma za msaada wa kisheria kama inavyoelekezwa.

Aidha  amesema kuwa migogoro itapungua sana iwapo mabaraza ya kata yatatekeleza majukumu yake kwa ufasaha hatua itakayowaondolea mzigo wanasheria wanaotekeleza jukumu hilo.

"Inafahamika kuwa migogoro inayoongoza nchini ni ya ardhi, ndoa na mirathi. Hivyo kwa kikao hiki tumekuja na mkakati wa kutatua migogoro hiyo kwa kuhakikisha kila mkoa tunakuwa na wanansheria wabobezi wawili watakaoshughulikia masauala hayo" amesema Wakili Odongo.

Katika namna hiyo hiyo Mkoa wa mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria amesisitiza uwajibika wa haki katika  kuwasaidia watoto, wanawake na makundi maalum.

Amepongeza mpango wa huduma za kisheria za SAMIA LEGAL AIDS  unaowaokoa maelfu ya wananchi wanyonge kupata haki ya kutatuliwa migogoro yao hususan ya ardhi ambayo ndio kinara.

Kwa upande wake Wakili Tamari Mndeme kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini, amesema wamegundua kuwa wananchi wote hawafanikiwi kumaliza migogoro yao katika kipindi cha kampeni ya  msaada wa kisheria unapotolewa, hivyo mpango mkakati ni kuwaimarisha wataalam wa sheria waliochaguliwa kusimamia migogoro ya wananchi kila mkoa bila malipo kuwasimamia wananchi mpaka pale watakapofanikiwa.

"Wananchi wengi wanaotafuta msaada wa kisheria uwezo wao kifedha ni mdogo, hivyo SAMIA LEGAL AIDS itawapatia msaada bure bila malipo hadi pale watakapofanikiwa, lengo la Rais wa awamu ya sita wa  jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuwarudishia wananchi tabasamu" amesema Wakili Tamari.



 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...