Farida Mangu, Morogoro

SERIKALI kupitia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi imeeleza kuwa itaendelea kutengeneza mahusuano na wananchi kwa ajili ya kudumisha misingi ya Amani.

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Denis Londo alieleza hayo wakati wa mazungumzo na mkuu wa mkoa Morogoro Adam Malima ofisini kwake.

Londo alisema katika kuendelea kudumisha mahusuano hayo na wananchi vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kusimamia suala la usalama wa raia na Mali zao.

"Wananchi waendelea kutengeneza mahusuano kati yao na Serikali wakati wa shida na Raha, na wavitegemee vyombo vya ulinzi katika kujenga Imani,ili shughuli zote za Maendeleo ziendelee kushika Kasi na wananchi waone matunda ya kazi na jitihada za Serikali yao,"alisema.

Alisema pamoja kufanya maboresho makubwa kwenye maeneo mbalimbali ya vyombo hivyo vya usalama ambavyo ni Polisi, Magereza, Uhamiaji, na Zimamoto.

"Kwa kazi ambayo uongozi wa mkoa wa Morogoro imeendelea kufanya ya kujenga Amani mmekuwa kinara na mfano kwa msingi wa mahusuano kati ya Wizara, vyombo vyetu na wananchi na hii ni katika kuleta Maendeleo,"alisema.

Londo aliwahakikishia wananchi kuwa kazi yao kama watendaji ni kumsaidia Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kwamba vyombo vya ulinzi na usalama wanavisimamia baada ya maelekezo yake.

Alisema vyombo hivyo ni vya wananchi ni ni vyema wananchi wakaendelea kuona matunda ya kazi na jitihada za Serikali yao.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima kwa upande wake alisema taasisi za vyombo vya ulinzi na usalama kwa mkoa wa Morogoro vimekuwa mfano wa kuigwa kwa kuimarisha suala zima la usalama.

Aidha kwa ukubwa wa mkoa wa Morogoro,Malima alisema kuwa kwa Sasa vimeanza kupatiwa vitendea kazi kama magari tofauti na ilivyokuwa awali kwani ilikuwa ni tatizo kufika baadhi ya maeneo.

"Kiusalama kwa ukubwa wa mkoa tuko vizuri, kuna maeneo bado tunahitaji maboresho zaidi na kuongezeja kwa vifaa mbalimbali ikiwemo majengo mfano Wilaya za Gairo, Malinyi na Kilosa majengo ya Magereza yanahitajika,"alisema.

Alisema upande wa Jeshi la Zimamoto imepatiwa magari mapya na kuondokana na changamoto zilizokuwa zikiukabili awali kwa kuwa na magari mabovu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwenye baadhi ya maeneo wamefufua maeneo ya kuchota maji pindi panapotokea majanga. huku kwa idara ya uhamiaji kujidhatiti kwa ulinzi na uingiaji wa wahamiaji haramu kupunguza.

Alisema mafanikio yaliyopo mkoa wa Morogoro ni kuhakikisha wananchi wanaishi kwa Amani na kuendelea kuimizana suala hilo wakati wote,jambo linalosaidia kufanya biashara zao na usimamizi kwa Mazingira wezeshi yenye Amani.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...