Serikali inaendelea na mkakati kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo katika suala la huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Kaimu Katibu Mkuu , Wizara ya Maji Bwn. Henry Chisute amesema akifungua Warsha ya uhakiki na Kujenga Uwezo, iliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.
Amesema Tanzania imepiga hatua nzuri katika eneo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira.
Amesema ongezeko la idadi ya watu, kasi ya miji kukua, na athari zinazoongezeka za mabadiliko ya tabianchi zinaendelea kuongeza shinikizo katika mifumo ya maji na usafi wa mazingira. Hivyo inalazimu kuendelea kuboresha na kuimarisha mbinu za kufikisha huduma kwa wananchi.
Ameainisha jitihada za serikali pekee hazitoshi kufikia ukubwa wa malengo hivyo ni muhimu sekta binafsi ishiriki kwa nguvu zaidi, kwa mpangilio mzuri na kwa ubunifu katika utoaji wa huduma, uwekezaji na uendelevu.
Ameongeza lengo la Serikali si kuhamisha jukumu kutoka taasisi za umma, bali ni kujenga mfumo imara zaidi ambapo wadau wa umma na binafsi wanajumuishwa katika kutoa huduma ya maji na usafi wa mazingira.
Warsha imehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali , Sekta binafsi na washirika wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, UNICEF, GIZ, AFD na KfW.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...