Na Mwandishi Wetu, WMTH – Dodoma

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ili kuwawezesha wadau wa sekta ya sanaa kufanya kazi zao kwa ubora na tija.

Waziri Kairuki ameyasema hayo tarehe 14 Januari 2026, alipofanya mazungumzo na mtengeneza maudhui ya mtandaoni, Bw. Vicent Pendael Njau maarufu kama KIREDIO, aliyefika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja upatikanaji wa huduma ya intaneti ya uhakika, fursa za kujipatia kipato kupitia mitandao ya kijamii, pamoja na uwepo wa sera na mifumo ya kiserikali ikiwemo ya kikodi inayogusa sekta ya ubunifu na maudhui ya mtandaoni.

Waziri Kairuki alimpongeza Bw. Njau (Kiredio) kwa kazi nzuri anayofanya na kutoa wito kwa watengeneza maudhui pamoja na wasanii kwa ujumla kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania pindi wanapotengeneza maudhui yao na kabla ya kuyaweka mtandaoni.

Kwa upande wake, Kiredio ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasikiliza vijana na kutambua mchango wao katika uchumi wa kidijitali, huku akiwasilisha changamoto mbalimbali zinazokabili sekta ya utengenezaji wa maudhui ili zifanyiwe kazi kwa wakati na kuiwezesha sekta hiyo kuendelea kukua.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Mohammed Abdulla pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.











Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...