Waswahili husema tembea uone na Mwenda bure si mkaa bure huenda ataokota.

Ukitaka kujaribu kuuokota mchanga unaohama njoo jirani na bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro ushangae.

Jirani na bonde hili la Olduvai kuna mchanga unaohama ambao huwavutia mealfu ya watalii kuja kujionea maajabu hayo.

Mchanga huu upo katika umbo la nusu mwezi na upo karibu na Bonde la Olduvai ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Mchanga huu wenye rangi nyeusi umetokana na madini ya chuma na majivu yaliyotokana na mlipuko wa Volcano kutoka Mlima Oldoinyo Lengai.

Mchanga huu ambao husogea kwa kasi ya takribani mita 15–29 kwa mwaka tuta lake lina urefu wa mita 5 na upana wa mita 100.

Hayo ndiyo maajabu ya Hifadhi ya Ngorongoro ukitaka kujua zaidi kuhusu mchanga huu tembea uone kwani fahari ya macho ni kuona na fahari ya macho haifilisi duka.

Tumerithishwa, Tuwarithishe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...