Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limeendelea na zoezi la utoaji wa elimu kwa wateja kwa kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  Wilayani Tunduru, kwa lengo la kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi na salama ya umeme majumbani na shuleni.

Katika ziara hiyo, TANESCO imetembelea shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Muungano na Shule ya Sekondari Frankwiston, ambapo Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Alan Njiro, amewapatia wanafunzi elimu kuhusu umuhimu wa kutumia umeme kwa uangalifu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya nishati hiyo.

Akizungumza na wanafunzi, Njiro amewahimiza kuwasaidia wazazi wao kupunguza gharama za umeme kwa kuzima taa na vifaa vya umeme wanapokuwa hawavitumii, Kwa  kuviondoa kwenye soketi, pamoja na kwenda kuwakumbusha wazazi wao kununua majiko ya umeme na vifaa vya umeme vyinavyotumia umeme kidogo (energy saver) ili kuepuka matumizi ya vifaa vinavyotumia umeme mwingi bila ulazima.

Aidha, wanafunzi wameelimishwa juu ya masuala ya usalama kwa kuonywa kuepuka kuchezea miundombinu ya umeme ikiwemo nyaya zilizo wazi, nguzo na transfoma, huku wakitakiwa kutoa taarifa kwa watu wazima au TANESCO mara moja wanapoona hitilafu yoyote ya umeme katika maeneo yao.

Kwa upande wa uongozi wa shule hizo ulipongeza juhudi za TANESCO Mkoa wa Ruvuma kwa kuwafikia wanafunzi na kuwapatia elimu hiyo muhimu, wakisema itawasaidia kuwa mabalozi wazuri wa matumizi salama na bora ya umeme katika familia na jamii zao kwa ujumla.

Zoezi hili ni sehemu ya mkakati wa TANESCO wa kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu matumizi sahihi ya nishati ya umeme, kupunguza gharama kwa wateja na kuongeza usalama, huku shirika likiahidi kuendelea na programu hiyo ya elimu katika shule na maeneo mbalimbali mkoani Ruvuma.



 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...