Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Ruvuma Alan Njiro, amesema kuwa umeme ni nishati muhimu lakini ni hatari endapo hautatumika kwa usahihi, kwani unaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii.

Njiro ameyasema hayo Januari 27 alipotembelea shule ya msingi Mwenge na Shule ya sekondari Nasuri iliyopo Wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya utoaji wa elimu ya matumizi salama ya umeme kwa wananchi na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,  kuhusu faida na athari za umeme.

Kwa mujibu wa Njiro, elimu hiyo inalenga kuwajengea wanafunzi uelewa mapema ili waweze kujilinda dhidi ya hatari za umeme na pia kuifikisha elimu hiyo kwa familia na jamii zao.

Ameeleza kuwa transfoma hutumika kupoza umeme kabla ya kusambazwa majumbani, hivyo ni hatari kwa mtu yeyote kuichezea au kukaribia miundombinu hiyo.

Njiro amewataka watoto kutoa taarifa kwa wazazi au walezi wao pindi wanapoona mtu akichezea transfoma au nyaya za umeme, ili hatua za haraka zichukuliwe, ameongeza kuwa ushirikiano kati ya TANESCO na jamii ni muhimu katika kuzuia ajali zinazoweza kujitokeza.

TANESCO Ruvuma imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kama sehemu ya mkakati wa kupunguza madhara yatokanayo na umeme, na kulinda miundombinu kwa kuzingatia  majukumu yake muhimu ya kuzalisha, kusafirisha, kusambaza na kuuza umeme nchini.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...