Na Mwandishi wetu, Simanjiro
WAKUU wa shule za sekondari na msingi wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamejengewa uwezo wa kuandaa taarifa za shule kutokana na kasi ya ukuaji na kuongezeka kwa matumizi ya sayansi na teknolojia ulimwenguni.
Wakuu wa shule 23 za sekondari, 110 wa msingi wa shule za serikali na binafsi wamejengewa uwezo wa kuandaa taarifa za shule ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa wake kupitia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Elimu.
Afisa elimu ya awali na msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Darius Daudi Limandola amesema walimu hao wamepata mafunzo hayo ya uandaaji wa taarifa za shule kwenye vituo vitatu vya Orkesumet, Terrat na Mirerani.
Limandola ameeleza kwamba mafunzo hayo ya mfumo wa utoaji wa taarifa za kielimu kupitia mfumo wa kidigitali (School Information System) una lengo la kurahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa za shule husika kwa wakati.
Ameeleza kwamba mfumo huo unafanyakazi katika kutoa taarifa za kielimu za shule husika kila siku ikiwemo hali ya miundombinu ya shule, utekelezaji wa lishe kwa wanafunzi, hali ya watumishi na upatikaji wa huduma nyingine za kijamii hususani maji na umeme.
Amesema wanufaika wa mafunzo hayo ni wakuu 23 wa shule za sekondari, walimu wakuu 110 wa shule za msingi, maafisa elimu kata, walimu wa taaluma na takwimu na maafisa elimu ngazi ya wilaya.
Amewataka walimu wakuu na wakuu wa shule kusimamia utekelezaji wa mfumo huo mara moja baada ya shule kufunguliwa Januari 13, 2026 ambapo utairahisishia serikali kufanya maboresho na maamuzi sahihi katika shule husika kwa wakati.
Mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo, afisa elimu vifaa na takwimu wa halmashauri ya wilaya hiyo, Abdalah Hamis amesema walimu hao wamejengewa uwezo kwa muda wa siku mbili na kisha watakwenda kuwaelekeza walimu waliobaki katika shule zao.
"Mafunzo yamefanyika katika vituo vitatu vya Orkesumet shule ya sekondari Simanjiro, shule ya sekondari Terrat na shule ya awali na msingi Glisten Mirerani, ambayo yameanza juu kwa wachache watakaokwenda kuwafundisha wengi," amesema Hamis.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, mkuu wa shule ya sekondari Tanzanite, Jude Samwel Mziray amesema mfumo huo ni mzuri kwani wanaaachana na mtindo wa kuingiza taarifa kwenye makaratasi na kuweka katika mfumo wa kiteknolojia.
"Mfumo huo unarahisisha kwani unatoa taarifa ya shule hadi ngazi ya kata, kisha wilaya hadi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) tofauti na tulivyozoea mwanzo kujaza katika makaratasi," amesema Mziray.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Naepo, kata ya Naisinyai, Simon Isack Magembe amesema mafunzo hayo yanawajengea uwezo zaidi wa kuboresha taarifa kwa matumizi sahihi.
Mwalimu Magembe amesema ujuzi walioupata wa kuandaa taarifa za mfumo huo umewarahisishia utendaji kazi wao tofauti na awali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...