Na Mwandishi Wetu
WANAFUNZI wa Chuo cha Kodi (ITA) wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Forodha kwa mjadala wa kitaaluma kuhusu jukumu la utendaji wa Himaya Moja ya Forodha (SCT) na Vituo vya Pamoja vya Forodha Mpakani (OSBP) katika kulinda jamii.
Akifungua maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza Chuoni, Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo amesema ITA inafanya shughuli za forodha kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wadau wake ya namna ya kukusanya mapato yatokanayo na forodha hivyo siku hii ni muhimu kwa ITA.
“Forodha pamoja na kukusanya kodi pia inalinda jamii kwa kuhakikisha kila bidhaa inayopita katika mipaka kuingia ndani ya nchi ni salama,” alisema Prof. Jairo na kuongeza kwamba Siku ya Kimataifa ya Forodha ni tukio muhimu kwani jukumu kubwa la forodha pia ni kulinda mipaka ya nchi.
Amesema kuwa Forodha ni eneo muhimu kwa Mamaka ya Mapato Tanzania kwani linakusanya asilimia 40 ya makusanyo ya TRA.
Katika hatua nyingine, Prof. Jairo amewataka wanafunzi wa ITA kuanzisha klabu ya Forodha ili kuendeleza taaluma ya Forodha kwani Chuo kinajitahidi kufundisha uhalisia wa masuala ya forodha hivyo ni jukumu la wanafunzi kuonyesha kwamba wamebobea.
Katika Mjadala wa kitaaluma wanafunzi wa Chuo cha Kodi wameelezwa tofauti kati ya Himaya Moja ya Forodha na Vituo vya pamoja Mpakani na kwa ujumla jinsi forodha inavyotumika kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inakuwa salama.
Msingi wa mjadala huo ni kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Forodha, isemayo,”Forodha Inalinda Jamii kwa Umakini na Kujitoa”.
Watoa mada katika mjadala huo walikuwa ni watumishi wa TRA ndugu Mbogo Kerenge na Ndugu Leonard Mutiba, mjadala ambao uliwapa fursa wanafunzi kuuliza maswali na kupata majibu ikiwa ni sehemu ya kuwapa uelewa zaidi wa shughuli za forodha.
Pamoja na Mkuu wa Chuo cha Kodi, maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Utawala, Mipango na Fedha Ndugu Emmanuel Masalu, Dk. Cyril Chimilia kwa Niaba ya Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Ndugu Mary Ruhara kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Forodha Chuo cha Kodi pamoja na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa ITA (ITASO), Ndugu Karimu Kitundu.
Wahadhiri wa masomo ya Forodha, wafanyakazi wengine wa Chuo pamoja na wanafunzi wa Chuo pia wameshirii wa mjadala huo.
Siku ya Forodha huadhimishwa kila Mwaka tarehe 26 Januari kwa kufanya shughuli mbalimbali ambapo ITA ikiwa ni mdau wa Forodha na Mwanachama wa Mtandao wa Kimataifa wa Vyuo vya Forodha (INCU) Vyuo Vikuu vya Forodha imeadhimisha kwa kajadiliana namna SCT na OSBP zinavyotumika katika Forodha..jpeg)
Afisa Forodha Mkuu Lenard mutiba akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa chuo cha kodi jijini Dar es salaam jana, wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Forodha kwa mjadala wa kitaaluma kuhusu jukumu la utendaji wa Himaya Moja ya Forodha (SCT) na Vituo vya Pamoja vya Forodha Mpakani (OSBP) katika kulinda jamii.
WANAFUNZI wa Chuo cha Kodi (ITA) wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Forodha kwa mjadala wa kitaaluma kuhusu jukumu la utendaji wa Himaya Moja ya Forodha (SCT) na Vituo vya Pamoja vya Forodha Mpakani (OSBP) katika kulinda jamii.
Akifungua maadhimisho hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza Chuoni, Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo amesema ITA inafanya shughuli za forodha kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wadau wake ya namna ya kukusanya mapato yatokanayo na forodha hivyo siku hii ni muhimu kwa ITA.
“Forodha pamoja na kukusanya kodi pia inalinda jamii kwa kuhakikisha kila bidhaa inayopita katika mipaka kuingia ndani ya nchi ni salama,” alisema Prof. Jairo na kuongeza kwamba Siku ya Kimataifa ya Forodha ni tukio muhimu kwani jukumu kubwa la forodha pia ni kulinda mipaka ya nchi.
Amesema kuwa Forodha ni eneo muhimu kwa Mamaka ya Mapato Tanzania kwani linakusanya asilimia 40 ya makusanyo ya TRA.
Katika hatua nyingine, Prof. Jairo amewataka wanafunzi wa ITA kuanzisha klabu ya Forodha ili kuendeleza taaluma ya Forodha kwani Chuo kinajitahidi kufundisha uhalisia wa masuala ya forodha hivyo ni jukumu la wanafunzi kuonyesha kwamba wamebobea.
Katika Mjadala wa kitaaluma wanafunzi wa Chuo cha Kodi wameelezwa tofauti kati ya Himaya Moja ya Forodha na Vituo vya pamoja Mpakani na kwa ujumla jinsi forodha inavyotumika kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inakuwa salama.
Msingi wa mjadala huo ni kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Forodha, isemayo,”Forodha Inalinda Jamii kwa Umakini na Kujitoa”.
Watoa mada katika mjadala huo walikuwa ni watumishi wa TRA ndugu Mbogo Kerenge na Ndugu Leonard Mutiba, mjadala ambao uliwapa fursa wanafunzi kuuliza maswali na kupata majibu ikiwa ni sehemu ya kuwapa uelewa zaidi wa shughuli za forodha.
Pamoja na Mkuu wa Chuo cha Kodi, maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Utawala, Mipango na Fedha Ndugu Emmanuel Masalu, Dk. Cyril Chimilia kwa Niaba ya Naibu Mkuu wa Chuo cha Kodi Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Ndugu Mary Ruhara kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Forodha Chuo cha Kodi pamoja na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa ITA (ITASO), Ndugu Karimu Kitundu.
Wahadhiri wa masomo ya Forodha, wafanyakazi wengine wa Chuo pamoja na wanafunzi wa Chuo pia wameshirii wa mjadala huo.
Siku ya Forodha huadhimishwa kila Mwaka tarehe 26 Januari kwa kufanya shughuli mbalimbali ambapo ITA ikiwa ni mdau wa Forodha na Mwanachama wa Mtandao wa Kimataifa wa Vyuo vya Forodha (INCU) Vyuo Vikuu vya Forodha imeadhimisha kwa kajadiliana namna SCT na OSBP zinavyotumika katika Forodha.
.jpeg)
Afisa Forodha Mkuu Lenard mutiba akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa chuo cha kodi jijini Dar es salaam jana, wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Forodha kwa mjadala wa kitaaluma kuhusu jukumu la utendaji wa Himaya Moja ya Forodha (SCT) na Vituo vya Pamoja vya Forodha Mpakani (OSBP) katika kulinda jamii.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...