
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania- TASAC Bw. Mohamed Salum leo tarehe 16 Januari, 2026 amehitimisha rasmi mafunzo kwa watumisi wapya 25 yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Wakati akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu amewaasa watumishi hao kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, nidhamu ya kazi, ushirikiano na ubunifu katika kazi.

“Ndugu watumishi, napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili katika utumishi wa umma, nidhamu kazini, ushirikiano na kuendelea kujifunza kwakuwa Sekta ya usafiri kwa njia ya maji inakuwa kwa kasi sana kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia” amesema Bw. Salumu.

Pia, amewasihi kuzingatia kanuni na miongozo katika kutekeleza majukumu yao.
“Napenda mtambue yakuwa mmepewa dhamana kubwa na serikali hivyo ni vema kuzingatia Kanuni, Sheria, Taratibu na Miongozo mbalimbali inayosimamia utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kutunza siri, nidhamu na utii kwa viongozi wa serikali, kuendeleza mashirikiano, kutoa huduma bora kwa wateja, kulinda mali za Shirika pamoja na kufuata sheria na miongozo inayoongoza utekelezaji wa majukumu ya TASAC.

Mwisho Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha watumishi wapya TASAC na kuwatakia utekelezaji mwema wa Majukumu yao.



Mafunzo yalikuwa ya siku 14 ambapo watumishi hao wali kabidhiwa vyeti vya ushiriki na kukaribishwa katika utumishi wa umma.

.jpg)





.jpg)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...