Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Prof.Peter Msofe amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri na Wataalam katika Wilaya nne zinazotekeleza mradi wa kuongoa ardhi na urejeshaji wa uoto wa asili wa IKI-FLR kusimamia kwa dhati na uadilifu mkubwa huku wakitoa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo ya mradi huo unaotekelezwa na Shirila la WWF na Wadau wenza.

Sambamba na kuwataka kuendelea kuhamasisha wananchi wa Wilaya hizo nne za Mikoa miwili ya Tanga na Dodoma ili waweze kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo pamoja na lengo la kupanda miti milioni moja na nusu kila mwaka Wilaya zote kuendelea kufanyiwa kazi kama inavyoelekezwa.

Prof.Msofe ameyasema hayo Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa mradi wa uongoaji wa ardhi na kurejesha uoto wa asili unaosimamiwa na wadau mbalimbali kufadhiliwa na Serikali ya Ujerumani.

Ambapo amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itakuwa mstari wa mbele kuunga mkono na kutoa ushirikiano kamili kuona mradi huu unaleta matokeo tarajiwa na hata zaidi ya pale inapowezekana.

"Wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa Halmashauri na wataalam wa zile Wilaya nne za mradi ,Niwaagize kwamba msimamie kwa dhati na kwa uadilifu mkubwa mradi huu huku mkitoa ushikiano wa kutosha kwa watekelezaji wa mradi ili kufanya shughuli zao kwa ustadi".

Aidha Prof Msofe ametoa Wito kwa wadau watekelezaji wa mradi huo WWF,WRI na IUCN kuhakikisha suala la uharibifu wa mazingira unadhibitiwa pamoja na kuhakikisha upotevu wa misitu unapungua kwa kiasi kikubwa.

"Nitoe Wito kwa wadau watekelezaji wa mradi huu WWF,WRI na IUCN hakikisheni suala la uharibifu wa mazingira unadhibitiwa na upotevu wa misitu unapungua kwa kiasi kikubwa kwani mmeshajipambanua Tanzania na Duniani kote kuwa ninyi ni Taasisi makini na madhubuti".

Awali akitoa salamu za Shirika la WWF Dkt. Lawrence Mbwambo amesema kuwa Shirika hilo lina miaka 60 tangu kuanzishwa kwake na katika kipindi chote hicho Serikali ya Tanzania imekuwa ikiwashika mkono katika utekelezaji wa majukumu yao ambayo imepelekea kudumu na mafanikio waliyonayo.

Naye Bwana Almas Kashindye akitoa Taarifa ya mradi amesema kuwa lengo la mradi huu ni kurejesha uoto wa asili katika maeneo ambayo yameharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu na za kiasili na pia wanataka kulinda na kuhifadhi bioanuwai ambayo itachangia kuboresha maisha ya wananchi wanaozunguka misitu.

Na kuongeza kuwa wameweka lengo la kurejesha uoto wa asili kwenye zaidi ya hekari elfu 40 za maeneo yaliyoharibiwa katika Wilaya 4 za mradi ambazo ni Tanga wilaya mbili ya Korogwe na Kilindi na Dodoma ni Mpwapwa na Chamwino.

Bwana David Kavishe akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma amesema kuwa wao kama Taasisi ya Serikali ni washirika muhimu katika utekelezaji wa mradi na asili ya jambo hili inatoka mwaka 2018 ambapo Serikali ya Tanzania iliridhia azimio la Umoja wa Afrika wa kuongoa ardhi iliyoharibika ambapo Tanzania iliahidi kuongoa hekari milioni 5.2 ya ardhi iliyoharibika.

Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 na utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.4 katika Wilaya nne kwa Mpwapwa na Chamwino mkoa wa Dodoma na kwa Wilaya ya Korogwe na Kilindi Mkoa wa Tanga.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...