FARIDA MANGUBE, MOROGORO

ZIARA ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba katika kata za Kidete na Tindika imekuwa faraja kubwa baada ya Serikali kutoa shilingi milioni 860 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji itakayoboresha maisha ya wakazi wa maeneo hayo

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Sospeter Lutonja, amesema kwa Kata ya Kidete vitachimbwa visima 6 vyenye thamani ya shilingi milioni 860, ambavyo vinatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 15,000.

Kwa upande wa Kata ya Tindika, serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika vijiji vya Tindiga A, Tindiga B, na Maluwi ambapo awali wakazi wa maeneo hayo walikuwa wakitumia visima vya mkono maarufu kama “visima vya mdundiko,” ambavyo havikutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.

Ziara ya Waziri Mkuu inaonesha wazi jinsi serikali inavyolenga kuhakikisha huduma za maji zinawafikia wananchi, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko na uhaba wa maji safi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...