Na WAF-Morogoro
Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa lisilo la kiserikali linalojikita katika kuongeza upatikanaji wa elimu kwa wasichana na kuwainua vijana wa kike kupitia elimu, uongozi na uwezeshaji wa kiuchumi (CAMFED) kwa mafunzo elekezi kuhusu miradi inayoisadia kufanikisha malengo na mipango yake kwa.ngazi ya msingi na taifa kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CAMFED Bi. Anna Sawaki amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa kiungo muhimu cha utekelezaji wa miradi ya afya na Shirika kwa kuendelea kuboresha mazingira ya afya mashuleni na kufungua fursa za ajira za sekta ya afya.
"Kupitia fursa za ajira zinazotangazwa na Serikali, Wizara ya Afya, jumla ya Wafadhiliwa 141 wa CAMFED wameajiriwa katika kada za ukunga na uuguzi," amesema Bi. Sawaki.
Ameongeza kuwa Wizara ya Afya na wafadhiliwa wanashiriki kwenye miradi kama vile School Water Sanitation and Hygiene (SWASH) inayolenga kutoa mafunzo ya usafi binafsi mashuleni, kuweka mbinu rafiki za kujikinga na mazingira hatarishi ikiwemo kupata ujauzito katika umri mdogo.
Aidha, amesema kuwa CAMFED itaendelea kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya ambapo ushirikiano huo unatekelezwa chini ya Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya pande hizo mbili, inayolenga kuunganisha juhudi za sekta ya afya na elimu ili kuhakikisha jamii inanufaika na huduma bora na endelevu za afya.
Wizara ya Afya na CAMFED zitaendeleza ushirikiano wao ambao ni ishara ya dhamira ya pamoja ya kuhakikisha huduma za afya ngazi ya msingi zinaimarika, huku jamii ikiwezeshwa kupitia elimu na maendeleo endelevu, ambapo malengo ya sasa ni kuanzisha huduma za ufadhili katika Halmshauri zipatazo 41 na kuunda jumla ya Halmashauri 76 zitakazotekeleza miradi hiyo.
Mafunzo hayo yametolewa Februari 19, 2026 Mkoani Morogoro, kwa Maafisa Habari wa Wizara ya Afya, Kilimo, Elimu Sayansi na Teknolojia, TAMISEMI, Vijana na Ajira, Maendeleo ya Jamii, na Maafisa Habari wa Halmashauri za Wilaya 35 za Mikoa 10 zinazotekeleza miradi hiyo.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...