§ Atoa siku kumi na tano wasiokamilisha malipo ya viwanja vinavyozunguka uwanja kukamilisha

 Asisitiza waliomilikishwa viwanja kufanya maendelezo

Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo tarehe 11 Februari 2026 ametembeleo eneo unapojengwa uwanja wa kisasa wa mpira kwa ajili Mashindano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) mkoani Arusha.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetekeleza Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi katika eneo lililopo pembezoni unapojengwa Uwanja wa mpira wa Afcon katika kata ya Olmoti Jiji la Arusha, mkoani Arusha.

Hata hivyo, pamoja na viwanja kuuzwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali lakini kuna baadhi ya waliochukua viwanja kushindwa kukamilisha malipo ndani ya muda huku baadhi waliomilikishwa wakishindwa kuendeleza maeneo yao.

Akiwa katika eneo la uwanja huo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo alijionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo ambapo alipongeza jitihada zinazofanyika za kuhakikisha uwanja huo unakamilika kwa wakati na hatimaye kutumika katika mashindano hayo makubwa ya Afrika.

Akigeukia wananchi waliochukua viwanja na kushindwa kukamilisha malipo kwa wakati, Mhe Akwilapo amewataka kuhakikisha wanafanya malipo ndani ya siku kumi na tano kuanzia tarehe 12 Februari 2026.

"Kuna wananchi walioomba viwanja katika maeneo yanayozunguka uwanja wa AFCON 2027 na kushindwa kukamilisha malipo ya viwanja hivyo, wanatakiwa kulipa ndani ya siku kumi na tano na baada ya hapo tutawanyang'anya na kuwapatia wengine". Amesema Akwilapo

Aidha, amesisitiza wananchi wenye hati milki za ardhi katika eneo linalozunguka uwanja huo kuhakikisha wanafanya maendelezo kwenye maeneo yao huku akiweka bayana kuwa, kama kuna mtu anayedhani hawawezi kufanya maendelezo katika muda wa kuelekea Mashindano ya AFCON 2027 basi airejeshe hati ili kupatiwa wale wanaoweza kufanya maendelezo.

Ujenzi wa mradi wa uwanja wa AFCON Arusha kwa sasa umefikia asilimia 74 na unatarajiwa kukamilika Julai, 2026.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa mpira unaotarajiwa kutumika katika mashindano ya mataifa ya afrika (AFCON 2027) jijini Arusha jana

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo (Kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Lucy Kabyemera wakipata maelezo ya mradi wa viwanja vinavyozunguka uwanja wa AFCON Arusha jana alipofanya ziara katika eneo hilo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo (wa tatu kulia) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Bi. Lucy Kabyemera (kushoto) wakielekea katika uwanja wa AFCON wakati wa ziara ya siku moja katika maeneo ya uwanja huo jana. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...