Baraza la Wafanyakazi la Sita la TMDA limefanyika kwa ufanisi tarehe 5-6 Februari, 2026 katika Manispaa ya Morogoro, kwa kuwakutanisha wajumbe wa Menejimenti na kutoka kwa Watumishi wa TMDA kwa lengo la kujadili na kukubaliana masuala mbalimbali ya kitaasisi yenye mchango mkubwa katika kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka.

Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Mpango Mkakati wa TMDA wa miaka mitano (2026/27 – 2030/31), Rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, pamoja na Mpango wa Mazingira, Jamii na Utawala (Environmental, Social and Governance – ESG).

Akifunga kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Dkt. Adam Fimbo, aliwashukuru wajumbe wa Baraza kwa maoni yao ambayo  yalilenga kujenga na yanayolenga kuboresha utendaji kazi wa taasisi, akisisitiza kuwa wafanyakazi ni sehemu muhimu ya TMDA na mchango wao ni nguzo ya mafanikio ya Mamlaka.

> “Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu la ushirikishwaji na uwazi katika maamuzi ya taasisi. Mawazo na maoni yenu yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mifumo ya utendaji na kulinda afya ya jamii,” alisema Dkt. Fimbo.

Baraza la Wafanyakazi la TMDA linajumuisha wawakilishi kutoka Menejimenti na Watumishi, na hukutana mara mbili kwa mwaka kwa mujibu wa sheria na miongozo ya utumishi wa umma. Lengo kuu la mikutano hiyo ni kujadili taarifa za utendaji kazi wa TMDA, kubaini fursa na changamoto zilizopo, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mifumo na huduma za Mamlaka.

Kupitia Baraza la Wafanyakazi, TMDA imekuwa ikiimarisha mshikamano, uwajibikaji na mawasiliano ya wazi kati ya Menejimenti na Watumishi, hali inayosaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa zingine zinazodhibitiwa, kwa lengo la kulinda afya ya jamii.

TMDA itaendelea kuthamini mchango wa Baraza la Wafanyakazi kama chombo muhimu cha ushirikishwaji katika maamuzi ya kimkakati na uendeshaji wa taasisi, sambamba na azma ya kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma bora kwa jamii.

Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza, Dkt. Adam Fimbo akifunga kikao na kuhitimisha Baraza la sita


Wajumbe wa Baraza wakufuatilia kikao
Mjumbe akitoa hoja katika kikao
Ushawishi katika utoaji maoni katika kikao
Usikivu kwa kila hoja inapowasilishwa
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza, Dkt.  FImbo akiongoza kikao kabla kufunga Baraza
Mjumbe wa kikao akiwasilisha hoja katika kikao
Ujuzi wa nguvu ya hoja katika uwasilishaji
Haki sawa katika kutoa maoni na kusikilizwa
Ufafanuzi katika masuala yaliyojadiliwa
Mbinu mbalimbali za Uwasilishaji wa hoja katika kikao



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...