Wafanyakazi wa Taifa Gas na wadau wengine wakiwa na furaha katika moja ya vituo karibu na kilele cha Mlima Kilimxanjaro kwenye zoezi la kupanda mlima baada ya kampuni hiyo kudhamini programu ya kutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi wa mazingira ambayo inaitwa “Guardians of the Peak” na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kampuni ya Kusambaza Nishati ya nishati safi ya kupikia ya Taifa Gas , mwaka huu 2026 imeweka historia kubwa kwa kuwa mdhamini mkuu wa programu kutangaza vivutio vya utalii na uhifadhi wa mazingira ijulikanayo kama 'Guardians of the Peak' ambayo ilikuwa na kauli mbiu “Embrace Clean Energy, Protect Tomorrow” na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kulinda mazingira.
Programu hiyo pia ilihusisha upandaji wa miti na kupanda mlima Kilimanjaro ambapo wadau mbalimbali walishiriki wakiwemo baadhi yaa wafanyakazi wa Taifa Gas ambao walihakikisha Chapa ya kampuni inafika kileleni mwa mlima kuashiria mafanikio ya safari ya uthubutu, mshikamano na dhamira thabiti ya kufikia malengo makubwa.
Tukio hilo linaweka alama ya historia katika juhudi za kuiinua chapa ya Taifa Gas katika viwango vya juu zaidi, kwa nguvu, umoja na kujituma kwa timu nzima ya wafanyakazi wa kampuni.
Mtungi wa Taifa Gas kuelekea kileleni mwa Mlima Kilimanjaro
Timu ya Wafanyakazi wa Taifa Gas ikiwa katika hatua za safari ya kupanda kuelekea kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, safari iliyojaa maandalizi, mshikamano na dhamira ya kupeperusha bendera ya kampuni katika paa la Afrika. Kupanda huku ni ishara ya uthubutu na ari ya kuendelea kufikia malengo makubwa



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...