Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma 

Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kimeiomba Serikali kurasimisha lugha ya alama ili iwe lugha rasmi ya mawasiliano Tanzania sambamba na Kiswahili na Kiingereza, kwa lengo la kuwawezesha watu wenye uziwi kuwasiliana na kupata huduma sawa na wananchi wengine.

 Mwenyekiti wa chama hicho Selina Edward, ametoa  ombi hilo wakati wa warsha ya pamoja katika ujumuishi wa watu wenye ulemavu, iliyofanyika Jijini Dodoma ikiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa serikali kurasimisha lugha ya alama kuwa sehemu ya lugha kuu za mawasiliano.

Amesema lugha ya alama ndiyo njia kuu ya mawasiliano kwa watu wenye uziwi na kuwa urasimishaji wake utasaidia kuondoa changamoto za mawasiliano kati ya viziwi na wasio na uziwi, hivyo kuwawezesha kupata haki za msingi kama wananchi wengine.

“Tumehangaika miaka mingi kuomba lugha ya alama irasimishwe na itumike kama lugha nyingine rasmi nchini,” 

 Amesema pamoja na kuwepo kwa sera inayotaka asilimia 30 ya zabuni za umma kutolewa kwa makundi yenye mahitaji maalum, utekelezaji wake bado ni mdogo kutokana na watendaji wengi kutofahamu sheria na sera husika.

 Mbunge wa viti maalum anayewakilisha watu wenye ulemavu, Nassiriya Nassir Ali, alisema ataendelea kupigania urasimishaji wa lugha ya alama ili kuwezesha ushiriki sawa wa watu wenye uziwi katika jamii.

Naye mshauri wa kisiasa kutoka Chama cha Viziwi cha Norway, Adriana Fjellaker, alisema ushirikiano wao na CHAVITA unalenga kusaidia viziwi kufahamu haki zao na kukuza ujumuishwaji wa kijamii.

Warsha hiyo ilihusisha viongozi kutoka serikalini, wadau wa maendeleo na wanachama wa CHAVITA, ikilenga kujenga uelewa kuhusu haki za watu wenye uziwi, kuimarisha mawasiliano jumuishi na kukuza ushiriki wa watu wenye ulemavu katika shughuli za kiuchumi.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...