Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeipongeza Sanlam Allianz kwa kuanzisha Mfuko mpya wa 'USD Fixed Income Fund' utakaowawezesha wawekezaji na wananchi kuweka akiba ya fedha za kigeni (sola ya Marekani).

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Mfuko huo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Masoko na Uchunguzi wa CMSA, Exaut Julius, alisema mfuko huo utachochea uchumi wa nchi na kuongeza akiba ya fedha za kigeni kwenye mzunguko.

"Tunawapongeza kwa kuzinduaa Mfuko huu kwa wakati muafaka kwani utachangia maendeleo yamasoko ya mitaji hapa nchini," alisema Julius.

Aidha, alisema Mfuko huo unaonyesha ushirikiano mzuri kati ya CMSA na wadau wake katika kukuza masoko endelevu na mitaji.

"Upatikanaji wa bidhaa bora za uwekezaji zinazoendana na viwango vya kimataifa ni nguzo muhimu katika kupanua ushiriki wa wawekezaji na kuendeleza masoko na mitaji hapa nchini," alisema Julius.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Muu wa kampuni hiyo, Jonathan Stichbury, alisema kuanzishwa mfuko huo ni hatua muhimu katika kuhamasisha utamaduni wa uwekezaji wenye tahadhari na kupanua fursa za uwekezaji zinazotumia dola ya marekani nchini Tanzania.

Alisisitiza pia dhamira yao katika kuzingatia uwazi, kufuata sheria na kanuni, pamoja na kuleta thamani ya muda mrefu kwa wawekezaji wote.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...