Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Kitanzania ya Compact Energies, inayojihusisha na uzalishaji na usambazaji wa vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati ya jua, imesema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia uwekezaji katika teknolojia za uzalishaji wa umeme wa jua kwa matumizi ya majumbani na viwandani.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa 5 wa Z-Summit Zanzibar uliomalizika hivi karibuni Visiwani Zanzibar, Meneja wa Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. Joseph Madata Biseko , alisema kuwa uwekezaji katika uzalishaji wa nishati ya jua utasaidia kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.

Aliongeza kuwa matumizi ya nishati ya jua yatasaidia pia kupunguza gharama za maisha kwa wananchi, kwa kuwa ni nishati nafuu na inayopatikana kwa uhakika ikilinganishwa na vyanzo vingine vya umeme vyenye gharama kubwa .

“Uzuri wa umeme wa jua, gharama ni wakati wa kuunganisha tu na hakuna malipo ya mwezi, ukitofautisha na aina nyingine ya nishati,”

“Kampuni yetu imejipanga kutoa suluhisho la changamoto za upatikanaji wa umeme usio wa uhakika kwa kusambaza vifaa vya ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu, ili Watanzania na wawekezaji wa kigeni wanufaike kupitia uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma mbalimbali,” amesema Bw. Biseko

Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta za utalii, uuzaji wa viwanja na nyumba, pamoja na nishati. Washiriki walitoka katika nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, Ghana, Nigeria, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kupitia jukwaa hilo, kampuni hiyo, iliyoshinda tuzo ya ‘Africa Company of the Year Awards’ katika kipengele cha Makampuni Makubwa Barani Afrika kutoka nchi 26 mwaka 2024, pia ilipata fursa ya kuonesha bidhaa na huduma zake, huku ikisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika nishati jadidifu kama msingi wa maendeleo endelevu ya kiuchumi nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...