Na Diana Byera,Kyerwa
MKUU wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Zaituni Msofe, amekabidhi rasmi nyumba kwa familia ya Jenifer Richard mwenye uhitaji maalum Mkazi wa Kakerere katika Kata ya Nkwenda iliyojengwa.
Nyumba hiyo imejengwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Devotha Daniel Mburarugaba ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kusaidia wananchi wenye uhitaji maalum.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Msofe amemshukuru Mbunge kwa kugusa maisha ya wananchi kwa vitendo, akielez hatua hiyo ni mfano wa kuigwa katika kuimarisha mshikamano na utu kwa jamii.
“Ninawapongeza viongozi wanaotumia nafasi zao kuleta matumaini kwa wananchi. Nawahimiza watu wote wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia wasiojiweza katika jamii yetu,” amesema Mkuu wa Wilaya Msofe.
Kwa upande wake, Mbunge Devotha Daniel Mburarugaba amesema aliguswa kuanza ujenzi wa nyumba hiyo baada ya kuona picha Mjongeo kupitia mitandao ya kijamii akiwa katika mazingira magumu ya maisha.
“Nilipoona hali aliyokuwa nayo, niliguswa na nikachukua hatua ya haraka. Leo tunashuhudia matokeo ya mshikamano na upendo,” amesema Mbunge huyo.
Aidha, Mbunge ameahidi pamoja na ujenzi wa nyumba hiyo, atahakikisha anakata bima ya afya kwa wote kwa familia yote ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu kwa uhakika na kwa wakati.
Hata hivyo Mbunge Devotha Mburarugaba pia amempongeza Raisa Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri yanayowezesha viongozi kuwahudumia wananchi na kusimamia maendeleo ya watu wenye mahitaji maalum.
Kwa niaba ya familia, ndugu wa karibu wametoa shukrani za dhati kwa Mbunge na uongozi wa Wilaya ya Kyerwa kwa msaada huo mkubwa ambapo wamefafanua walikuwa wanaishi katika mazingira magumu kwa muda mrefu.
Hivyo nyumba hiyo ni mwanzo mpya wa maisha yao na imewarejeshea matumaini na heshima katika jamii. Walimuombea Mbunge na viongozi wote waliohusika baraka na mafanikio katika kuendelea kuwahudumia wananchi.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...