Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ameanika hadharani kile kinachoonekana kuwa ni ukaidi na kusuasua kwa utendaji kazi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, baada ya maelekezo ya mfululizo ya serikali kuhusu usalama wa umma kupuuzwa kwa takriban nusu mwaka.
Katika hali inayoashiria kuvurugika kwa nidhamu ya kazi na mnyororo wa amri (chain of command), Mhe. Kasilda amewapa viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo makataa ya saa 72 kueleza kwa maandishi sababu za kushindwa kutekeleza agizo la kuvunja jengo la Soko Kuu la Same ambalo ni hatarishi.
Akizungumza kwa ukali mara baada ya kutembelea soko hilo, Mkuu huyo wa Wilaya alishangazwa na ukimya wa watendaji hao huku jengo hilo likiwa na nyufa kubwa zinazotishia maisha ya wananchi.
Alibainisha kuwa mkwamo huo si wa rasilimali, bali ni wa kinidhamu.
"Huu ni ukaidi wa wazi. Nimeshatoa maelekezo zaidi ya mara tatu kuhusu kuvunjwa kwa jengo hili, lakini hakuna utekelezaji.
Inasikitisha zaidi kuona hata barua rasmi ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) iliyoandikwa tangu Agosti 2025 imepuuzwa kwa miezi sita sasa," alisema Mhe. Kasilda.
Kauli hiyo ya DC Kasilda inaibua maswali mazito juu ya namna watendaji wa chini wanavyochelewesha maamuzi ya viongozi wa juu, hali inayoweza kuhatarisha usalama wa wananchi wanaotumia jengo hilo lililodumu kwa zaidi ya miongo mitano.
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwa serikali haiwezi kuvumilia utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea, hasa unahusisha hatari ya maafa.
Amewataka wahusika wote waliohusika kukwamisha agizo hilo kutoa utetezi wao kabla ya hatua kali za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yao.
" Nataka maelezo ya maandishi ofisini kwangu kueleza kwanini maelekezo ya serikali yanadharauliwa.
Hatua za kinidhamu zitafuata kwa kila aliyeshiriki kukwamisha jambo hili," alionya DC Kasilda.
Tukio hili linatathminiwa na wadau wa utawala bora kama fundisho kwa watendaji wa umma wanaoshindwa kutekeleza wajibu wao kwa wakati, huku likionyesha dhamira ya Mkuu huyo wa Wilaya katika kusimamia uwajibikaji bila muhali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...