WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa ajili ya kupitia hatua mbalimbali zilizofikiwa katika maandalizi ya michuano hiyo mikubwa itakayofanyika mwaka 2027 katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amefanya kikao hicho leo Jumanne (Februari 10, 2026) Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu amepongeza kazi kubwa inayofanywa na kamati hiyo, akieleza kuridhishwa na kasi na mwelekeo wa maandalizi yanayoendelea.

“Maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa yanaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji bora wa michuano hiyo”.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ni muhimu kuwepo kwa ushirikishwaji wa sekta zote, “mawaziri, makatibu wakuu pamoja na watendaji wengine hakikisheni mnazishirikisha sekta zetu kila mmoja katika eneo lake, tunataka kuona matokeo chanya katika michuano hii”.

Aidha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewataka wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha kila mmoja anasimamia kikamilifu eneo lake la uwajibikaji, ili hatua zote za maandalizi zikamilike kwa muda uliopangwa na kwa viwango vinavyokubalika.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...