-Ataka uchunguzi wa matumizi ya fedha na ununuzi wa vifaa hospitalini hapo.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 14, 2026 ameweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya Kilindi iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.64 ambapo kati ya fedha hizo shilingi 2.51 ni kutoka Serikali Kuu, Shilingi milioni 50 ni za mapato ya ndani ya Halmashauri na shilingi milioni 89.9 ni kutoka Benki ya Dunia 

Ujenzi wa Hospitali hiyo umesaidia kuwapunguzia  wananchi adha na gharama kubwa za matibabu ambazo walilazimika kuzifuata katika Wilaya za jirani.

Pamoja na kuridhishwa na ubora wa majengo katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amemtaka Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga kufuatilia na kujua ni kwanini idadi ya majengo yaliyopo ni machache kuliko yaliyokusudiwa ikiwa fedha yote ya utekelezaji wa mradi ilitoka.

“Majengo yapo kwenye viwango vizuri, ila fedha iliyokuja ilikuwa ijenge majengo mengi zaidi lakini mmejenga pungufu, fedha nyingine ipo wapi?, michezo ya upotevu wa fedha za Serikali hatuwezi ivumilia”








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...