Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Februari 2026, Dodoma.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amewahimiza watendaji DSE kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika masuala ya masoko na kuendelea kuvutia uwekezaji.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, ameahidi kuendelea kushirikiana vema na Serikali katika kutafuta mitaji ili kuweza kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni Moja ifikapo 2050.

Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ni taasisi ya kimkakati ya Taifa inayowezesha ukusanyaji na usimamizi wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kufadhili maendeleo ya uchumi wa Tanzania. DSE ni jukwaa rasmi linalowawezesha wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kufanya biashara ya hisa, hatifungani, na bidhaa nyingine za kifedha katika mazingira yenye uwazi na utawala bora.

Thamani ya Jumla ya Soko la Hisa la Dar es Salaam ni shilingi Trilioni 31.9, ikiwa na jumla ya wawekezaji waliosajiliwa 779,000

Soko la Hisa la Dar es Salaam ni Mwanachama wa Masoko ya hisa ya Dunia, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...