MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, ENOCK KOOLA, ametembelea Soko la Makuyuni lililopo Mji Mdogo wa Himo, Kata ya Makuyuni, kwa lengo la kukagua hali ya miundombinu ya soko hilo wakati wa msimu wa mvua pamoja na kukabidhi matenki mawili ya lita elfu kumi kila moja.
Ahadi hiyo ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 baada ya kupokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara.
Akizungumza na wafanyabiashara na wananchi waliojitokeza sokoni hapO Mbunge alisema upatikanaji wa maji ni suala la msingi katika kulinda afya ya umma, hadhi ya wafanyabiashara, na usalama wa chakula.
Katika hatua nyingine, Mbunge alikagua hali ya usafi wa soko na kubaini uwepo wa taka zilizorundikana katika vizimba vya kuhifadhia taka.
Mbunge, ameeleza masikitiko yake juu ya hali hiyo na kutoa muda wa saa 24 kwa Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kuhakikisha taka zote zimeondolewa na eneo la soko kurejeshwa katika hali ya usafi.
"Hali hii ni hatari kwa afya za wananchi hivyo kama mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo la Vunjo sipo tayari kuvumilia na kuona hali hii. Naomba taka zote ndani ya saa 24 zisiwepo." Alisema Koola.
Afisa Mazingira alipokea maelekezo na kuahidi kutekeleza agizo hilo na ndani ya muda uliopangwa.


.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...