Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne, huku baadhi ya wanafunzi wakifutiwa matokeo yao kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu, ikiwemo kuandika matusi katika karatasi za mitihani.
Wakati baadhi ya wanafunzi wakikumbana na adhabu hiyo, hali imekuwa tofauti kabisa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari FEZA Boys, ambapo matokeo yao yameleta furaha kubwa.
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa, jumla ya wanafunzi 71 walifanya mtihani wa Kidato cha Nne katika shule hiyo. Kati yao, wanafunzi 69 wamepata ufaulu wa Daraja la Kwanza (Division I), huku wanafunzi wawili pekee wakipata Daraja la Pili (Division II).
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Said Hassan, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa siri ya mafanikio hayo ni ushirikiano wa pamoja kati ya wazazi, walimu na wanafunzi, mkakati wanaouita “Utatu Mtakatifu (W3)”.
Alisema kuwa kwa upande wa shule, walimu hutimiza wajibu wao kwa kufundisha kwa bidii, huku wazazi wakipewa jukumu la kuhakikisha mahitaji muhimu ya wanafunzi yanapatikana kwa wakati, hali hiyo humwezesha mwanafunzi kupata muda wa ziada wa kujisomea.
Aidha, shule hiyo ina utaratibu wa kukaa na wanafunzi mmoja mmoja ili kufahamu changamoto zao, jambo linalosaidia kujenga urafiki kati ya mwalimu na mwanafunzi na hivyo kuongeza hamasa ya kupenda masomo.
Pia, shule hufanya mitihani ya mara kwa mara, ikiwemo kwa kushirikiana na shule jirani, hali inayowasaidia wanafunzi kuzoea mitihani na kuichukulia kama jambo la kawaida.
Kwa upande wa wanafunzi bora, Baraka Yunus, aliyepata alama A katika masomo yote, alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi za pamoja kati ya shule na wazazi, aliongeza kuwa alipata muda wa kutosha wa kusoma akiwa shuleni na anatarajia kuwa mfanyabiashara baada ya kumaliza masomo yake.
Naye Chriss Mwingila, ambaye pia alipata alama A katika masomo yote, aliwashukuru walimu na wazazi kwa kuwawekea mazingira rafiki ya masomo yaliyowasaidia kupata muda wa kutosha wa kujifunza
Waalimu na wanafunzi wa shule ya Feza Boyz wakishangilia mara baada ya kupata matokeo ya kidato cha nne na kupata ufaulu wa alama A kwa darasa zima
Mwalimu wa taaluma wa shule ya Feza Boyz ,Said Hasan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wa shule ya Feza Boyz wakishangilia kwa kuwabeba wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne na kupata ufaulu wa alama A kwa darasa zima

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...