Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BARAZA la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limesema limejipanga kutekeleza mambo yote muhimu yaliyowasilishwa na kamati za baraza hilo kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi wa Jiji hilo lenye idadi kubwa ya watu nchini.
Kupitia kikao cha Baraza la Halmashauri hilo kilichofanyika Februari 24,2025 chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilali kimetoa muelekeo wa yale ambayo yanakwenda kufanyika katika kata zote 36 kupitia maazimio yaliyopitishwa na kikao hicho.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa kikao hicho ambacho kulikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo ya kupokea taarifa ya robo ya pili ya mwaka kuanzia Oktoba hadi Desemba 2025 ,Meya Bilali maarufu kwa jina la Shetta amesema baraza hilo limekutana katika kikao cha kawaida lakini amewahakikishia wananchi kuwa kuna mambo ya msingi wameazimia kuyatekeleza kwa maendeleo ya Jiji hilo.
“Mabaraza kama hayo ni ya kawaida kwa lengo la kuhakikisha ajenda zinapitishwa haswa kwa kutambua tumetoka katika vikao vya bajeti.Kimsingi mabaraza hayo yanasaidia katika utekelezaji, pia kurahisishia watendaji na madiwani kwenda kusimamia ambayo wamekubaliana katika baraza.”
Meya Bilali amesema matarajio ya wananchi ni makubwa katika baraza hilo ambalo ni wazi viongozi wote hasa madiwani wamekuwa na shauku ya kusimamia na kuleta maendeleo ndani ya kata zao 36.
“Niwahakikishie wananchi wa Jiji la Dar es Salaam tunakwenda kusimama nanyi katika kuhakikisha tunatekeleza mambo mbalimbali yanayokwenda kutekelezwa katika jiji hilo.Wananchi tegemeeni mambo mazuri katika jiji la Dar es Salaam.”
Pamoja na hayo Meya Bilali amefurahishwa na ushiriki wa vyama vya upinzani vya ACT-Wazalendo na CHAUMA katika kikao cha baraza hilo ambapo amesema uwepo wa vyama hivyo ni chachu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kufanya vizuri
Awali wa kamati wa kikao cha baraza hilo kamati mbalimbali za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zimewaslisha taarifa zao za kuanzia Oktoba hadi Desemba 2025 sambamba na kutoa maazimio kadhaa.
Kwa upande wa Kamati ya Mipango Miji nq Mazingira ambayo Mwenyekiti wake ni Diwani wa Kata ya Kariakoo Haji Manara pamoja na mambo mengine imetoa maazimio kuwa katika Jiji hilo ziwe na mifereji ya kupitisha maji ili kusaidia barabara hizo kudumu kwa miaka mingi.
Azımio lingine kamati hiyo ni kwamba miradi ya ujenzi iwe shirikishi katika kata husika kwani hivi sasa unaweza kukuta kibali cha ujenzi kimetolewa lakini kata haina taarifa.Hivyo yeyote ambaye atakuwa na kibali cha ujenzi ahakikishe nakala ya kibali hicho inapelekwa eneo husika .
Wakati Kamati ya Utawala na Fedha nayo umewasilisha taarifa yake ya utekelezaji katika kikao cha baraza hilo sambamba na kutoa maazimio kadhaa likiwemo la fedha zinazotengwa katika miradi ya miundombinu hasa barabara iongezeke kutoka asilimia 10 mpaka asilimia 15.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...