WAKATI Chama Cha Mapinduzi(CCM) leo Februari 5,2026 kikitimiza miaka 49 tangu kuanzishwa kwake Februari 5,1977 wanachama, mashabiki, wapenzi na wadau mbalimbali wameungana na Chama hicho katika kusherekea.
Hata hivyo pamoja na kuadhimisha kwa sherehe hizo Kada wa Chama Cha Mapinduzi na mdau wa maendeleo nchini, Nathan Kimaro ameungana na Wana CCM kusherekea miaka 49 ya Chama hicho ambapo pia ametoa ushauri wenye lengo la kujenga Chama imara zaidi.
Katika ushauri wake anesema kila taasisi kubwa hufika wakati wa kujitathmini. Hivyo siku hii iwe si ya kusherehekea miaka pekee, bali ya kuhuisha dhamira.
Amesema "Wakati umefika tuwe ni Chama ambacho unyenyekevu uwe dira yetu chama cha kutoa matumaini, kurejesha furaha, na kuacha alama ya Utu,Huduma na kusimamia haki na stahiki za wananchi.
"Tuiunganishe nchi yetu, tuwe sehemu ya mchakato wa uponyaji, na tuwape watu sababu ya kutabasamu tena.
"Ni wakati wa kurudisha kwa wale waliotuamini kwa miaka yote, 𝗸𝘄𝗮 𝗞𝘂𝗮𝗻𝘇𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗖𝗖𝗠 𝗙𝗢𝗨𝗡𝗗𝗔𝗧𝗜𝗢𝗡."
Amesema Foundation hiyo ya Chama ni kwa ajili ya kuwahudumia wasio na sauti, kukuza vijana, wanawake, haki za watoto, elimu pamoja na kusaidia wagonjwa,yatima, wajane, na wanaoonewa.
Pia kutoa misaada ya kimaisha, na kuleta uso mpya wa CCM kwamba sio tu jukwaa la siasa pia Chama cha huduma kwa watu wa kada zote.
"Nyimbo mpya si nyimbo za majivuno au mashindano na kiburi, kama “CCM ni ile ile” au “wachawaseme CCM ina wenyewe” bali nyimbo za uzalendo, motisha, na maendeleo,nyimbo zitakazolisukuma kilimo na kauli mbiu za Umoja.
"Tuvae katika uvaaji wa ukaribisho na urafiki, tuwatazame upande wa pili kwa jicho la tabasamu na hata wanapokosea kwa mipango miovu na ukosofu wa Nidhamu, CCM Kama chama Baba na Mama kiwatazame kwa jicho la Mlezi kwa Mtoto mkosaji,
"Tujenge chama chenye umoja na nidhamu ya ndani. Kwa njia hii, CCM haitabaki kuwa historia bali itaendelea kuwa ahadi hai ya taifa. Na kuyaishi maneno ya Baba wa Taifa ya CCM madhubuti.
Heri ya Siku ya Kuzaliwa chama changu CCM."

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...