CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimesema kimeridhishwa na ujenzi wa mradi wa kituo cha kupooza umeme kilichopo Ziba wilayani Igunga mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM taifa Kenani Kihongosi alisema hayo alipokagua ujenzi wa mradi huo uliogharibu shilingi bilioni 5.8 ambazo ni fedha za ndani kutoka Shirika la Umeme nchini TANESCO katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani Tabora.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa laini tano za matoleo ya umeme, ujenzi wa miundombinu ya umeme pamoja na ofisi ya kudhibiti mifumo ya vifaa vya umeme, ujenzi wa kibanda cha walinzi ulinzi wa uzio wa kituo.
Awali Kihongosi alikagua mradi wa ujenzi wa shule ya Awali na Msingi Ibologero unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 342.
Komredi Kihongosi alisifu jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga shule za viwango na madarasa ya kisasa akiwataka wananchi hao kuwapeleka watoto shule wakapate elimu.


















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...