Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema maendeleo ya mradi wa ukarabati wa Meli ya MV Liemba mkoani Kigoma yanaridhisha na utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 55.
Kihenzile amesema hayo leo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Kigoma ambapo Naibu waziri huyo ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati huo na kusisitiza umuhimu wa meli hiyo katika kuchochea uchumi na kurahisisha usafiri katika Ziwa Tanganyika.
Aidha, Kihenzile amepata fursa ya kutembelea boti ya utafutaji na uokoaji iliyonunuliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania. Alifafanua kuwa boti hiyo itasaidia kuongeza uwezo wa kukabiliana na ajali za majini, matukio ya dharura pamoja na vitendo vya uhalifu katika Ziwa Tanganyika.
Pia Naibu waziri huyo ameeleza kuwa uwekezaji huo una lengo la kuimarisha usalama wa wasafiri na mali zao, sambamba na kuboresha huduma za usafiri majini, huku akisisiitiza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya usafiri ili kuhakikisha sekta hiyo inachangia kikamilifu maendeleo ya taifa.
Katika hatua nyingine, Kihenzile ametembelea mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege mkoani humo, ambapo utekelezaji wake unaendelea vizuri na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika miradi yote aliyokagua na kuwataka wasimamizi kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
.jpeg)



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...