Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Reuben Kwagilwa, amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni, mradi unaolenga kuondoa changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.
Mhe. Kwagilwa amefanya ukaguzi huo leo Februari 10, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi hospitalini hapo, ambapo alipata fursa ya kujionea hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo pamoja na maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa.
Katika ziara hiyo, alipokea maelezo ya kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri kuhusu maendeleo ya ujenzi, hali ya utekelezaji wa mradi pamoja na matarajio ya kukamilika kwake.
Ujenzi wa jengo hilo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya afya, kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi pamoja na kuongeza uwezo wa hospitali kutoa huduma za dharura na kuokoa maisha ya wagonjwa.
Jengo hilo la kisasa linatarajiwa kuwa na mfumo wa hewa tiba (Oxygen) pamoja na vifaa maalum vya ufuatiliaji wa wagonjwa mahututi vitakavyowezesha uangalizi wa karibu wa hali zao.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...