Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Dennis Londo amelitaka Baraza la Wafanyakazi la Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuwa chachu na sehemu ya suluhisho katika kuongeza tija, kuchochea ubunifu na kuongeza ufanisi wa Shirika .
Wito huo umetolewa mapema leo akiwa mgeni rasmi Mkoani Morogoro wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa TBS.
Mhe.Londo alisema baraza hilo linapaswa kuwa chombo chenye mchango chanya katika kuboresha mazingira ya kazi, kuimarisha ustawi wa wafanyakazi, na kuongeza ufanisi wa Shirika katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria.
Alisema TBS ina jukumu nyeti la kuhakikisha bidhaa na huduma zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vya ubora, usalama na ushindani katika masoko ya.ndani na ya kimataifa.
Alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua na kuthamini nafasi ya Mabaraza ya Wafanyakazi kama vyombo muhimu vya kisheria vinavyolenga kuimarisha mahusiano mema kazini, kukuza majadiliano ya kijamii, na kuhakikisha haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi vinatekelezwa kwa uwiano na kwa maslahi mapana ya taasisi na Taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...