Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro jana tarehe 26 Februari 2026 limepokea ugeni mzito uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Mhe. Patrobas Paschal Katambi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Jacob Jack Mwiimbu pamoja na ujumbe wa wageni 70 wa majeshi ya ulinzi na usalama waliopo nchini kwa majukumu mbalimbali na kufanya utalii hifadhi ya Ngorongoro.

Waheshimiwa mawaziri na Ujumbe wao waliopata fursa ya kutembelea vivutio vilivyopo Ngorongoro na kushuhudia Wanyama wakubwa watano (Simba, Chui, Nyati, faru na Tembo), makundi ya Pofu, pundamilia, swala, Nyumbu, Ngiri, Viboko, ndege, mimea ya asili, kasoko ya Ngorongoro na kupata simulizi mbalimbali kuhusu utalii wa miamba na hadhi tatu za kitamaifa zilizopo Ngorongoro.

Mhe. Katambi ameipongeza Ngorongoro kwa uhifadhi unaozingatia usalama wa mazingira, kulinda fahari ya Ngorongoro kama kivutio bora cha utalii Afrika.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...