Na Said Mwishehe,Michuzi TV

HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam limezindua programu maalumu ya Eco School kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari  yenye lengo la kujenga uelewa wa utunzaji na Uhifadhi wa mazingira kwa vijana na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza leo Februari 27,2026 wakati wa uzinduzi wa programu ya ECO School uliofanyika katika Shule ya Sekondari Juhudi ,Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Edward Mpogolo amesema programu hiyo imekuja wakati muafaka.

“Programu hii iwekewe mkakati wa kuitekeleza na niwapongeze Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuja na mpango huu kwani inaonesha namna mnavyothamini na kutambua ukuu wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji wa mazingira .

“Pia Halmashauri mnatambua juhudi za Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan alivyokuwa mpambanaji namba moja wa mazingira ,dunia ilimtambua na ikampa tuzo.Hivyo halmashauri kuwa na programu ya Eco School pamoja na muongozo wake wa namna ya kuutekeleza mmefanya jambo kubwa…

“Mmefanya jambo kubwa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuamua mpango huu kuupeleka kwa watoto wadogo ni namna mnavyorithisha utunzaji wa mazingira.Ni ishara njema ya kufanya jambo hili kuwa endelevu,”amesema .

Pia amesisitiza fedha zinazotengezwa kwa ajili ya mazingira zitumike katika utunzaji wa mazingira badala ya fedha hizo kuzipeleka katika miradi mingine .”Fedha zinazotengwa kwa ajili ya mazingira zitumike katika mazingira.”

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amesema Halmashauri ya Jiji hilo linakuwa kwa kasi sana, hivyo inatafsiri katika shughuli za binadamu inachukua shughuli kubwa katika maisha yetu hivyo suala la mazingira hauwezi kuliacha au kulitenganisha 

Ameongeza wazo hilo  limekuwa muafaka katika mipango yao ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kwamba halmashauri imeendelea kutenga fedha kwa maana ya eneo hili la mazingira katika elimu msingi na sekondari 

“Katika asilimia 70 tunayopeleka katika maendeleo ukichukua asilimia 40 inakwenda kwenye elimu ya sekondari na msingi pamoja na miundombinu lakini tunataka tuongeze na eneo hili la mazingira ambalo ni muhimu na ndio muelekeo wa Serikali.

“Hivyo tunaamini kwa mpango wa Eco  School utatusaidia kufanikisha utunzaji wa mazingira ikiwemo uondoshaji wa taka na katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha mwaka 2021/2025 jumla ya miti milioni 2.7 ilipandwa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.”

Aidha amesema lengo la Eco School ni kubadilisha mtazamo wa vijana na wananchi katika uhifadhi wa mazingira lakini pia kuhakikisha uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya elimu unakuwa endelevu 

“Kwa kuzingatia program hii halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itatekelezwa katika shule 10 ambazo ni Kitunda Relini , Bunatra, Ukonga,Kitunda , Minazi Mirefu, Misitu, Kivule Sekondari ,Kirezange sekondari ,Saranga na Mvuti.Katika kufanikisha lengo hilo leo hii tunazindua programu ya Eco School.

Amefafanua programu hiyo itajikita katika utenganishaji na urejeshaji wa taka,upandaji na utunzaji wa miti, bustani za maua,uvunaji wa maji ya mvua, matumizi ya nishati ya biogesi ,nishati ya umeme jua na nishati safi ya kupikia.

Pia amesema wamezindua muongozo wa Eco School ambao halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lakini kwenye Wilaya ya Ilala watautumia katika uendelezaji wa programu hii katika halmashauri yetu 

Wakati huo huo Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilali maaru Shetta amesema ameoneshwa kufurahishwa na programu hiyo ambayo inakwenda kuwajengea uwezo wa watoto katika utunzaji wa mazingira. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...