Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika Kata ya Saranga, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuhakikisha wananchi wanapata miundombinu bora na huduma zinazokidhi mahitaji yao ya kila siku.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Kairuki alitembelea Barabara ya King’ongo, kipande cha urefu wa mita 200 kilichopo karibu na Ofisi ya TRA Kimara Mwisho, ambacho kinajengwa kwa kiwango cha zege.
Barabara hiyo inatarajiwa kuboresha usafiri na kuongeza usalama kwa wananchi wanaoitumia.
Aidha, Mbunge huyo alikagua pia Barabara ya Suka Golani yenye urefu wa kilometa 1.5, ambayo imechongwa kwa kujazwa kifusi na kushindiliwa, hatua inayolenga kurahisisha upitishaji wa magari pamoja na kuboresha shughuli za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Kairuki alipata fursa ya kuwasikiliza wananchi wa Kata ya Saranga waliowasilisha kero zao mbalimbali, hususan changamoto ya uhaba wa vivuko salama katika baadhi ya maeneo.
Mbunge huyo alisifu moyo wa ushirikiano uliooneshwa na wananchi waliokwisha anza kuchangia ujenzi wa baadhi ya vivuko, na kuahidi kutoa sapoti ili kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Vilevile, Mheshimiwa Mbunge alitembelea Mtaa wa Upendo, ambako wananchi walieleza hamu yao ya kuona ujenzi wa shule katika mtaa huo ili kusogeza huduma ya elimu karibu na watoto wao.
Ziara hiyo imeacha faraja na matumaini mapya kwa wananchi wa Kata ya Saranga, ambao wameonesha imani yao kwa uongozi wa Mbunge wao na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...