Mbunge wa Jimbo la Katoro injinia Kija Limbu Ntemi Leo ametoa sadaka ya tende katika misikiti mbalimbali ya Jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya kudumisha umoja na amani kama desturi ya Watanzania
Injinia kija alisema kuwa ataendelea kusimamia suala la mshikamaano na kuhakikisha Kila mwananchi ana uhuru wa kuabudu kwa Imani yake.
Katika hatua nyingine mbunge huyo ameahidi kununua vitabu kwa ajili ya watoto wa kiislam mashuleni, vitabu ambayo vimetajwa kuwajenga watoto hao katika misingi Bora.
Akizungumza kwa niaba ya waumini hao imamu wa msikiti wa Islamiya ostadhi Najimu Amry ameomba uongozi wa mtaa kusimamia wamiliki wanaofuga wanyama aina ya ngurue kuwafungia ili isiwe kero kwa wananchi wengine ambao wameharamishwa mnyama huyo.
Nae diwani wa kata ya Katoro Zubeda Mohamed ameshiriki zoezi la utoaji sadaka hiyo katika msikiti wa Al masjid Hudaa wa kata ya Katoro.
Kwa upande wake sheikh wa kata ya Katoro Muhammad Salimu Mwanchonga amemshukuru mbunge huyo kwa kupeleka sadaka hiyo katika misikiti mbalimbali ya Jimbo Hilo.
Sambamba na Hilo Waumini wa msikiti wa islamiya uliopo kata ya Ludete wamemlalamikia mbunge wa Jimbo la Katoro juu ya uzurulaji wa mifugo aina ya Ngurue wanaozagaa hadi katika maeneo ya msikiti.
Wametoa malalamiko hayo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Katoro Eng Kija Limbu Ntemi wakati alipoenda kutoa sadaka ya tende kwa ajili ya futuru katika misikiti ya kata mbali mbali ya Jimbo la katoro.
Akijibu malalamiko hayo injinia Ntemi ameahidi kulifikisha suala Hilo katika halmashauri ili liweze kutatuliwa kwa haraka bila kuwa kero kwa mtu yoyote.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...