Katika msimu huu wa sikukuu ya wapendanao (Valentine Day) hauna haja ya kwenda porini kuhangaika kutafuta mchawi wa kukusaidia kustawisha penzi lako kama liko mashakani, dawa ya kuimarisha penzi ni ndogo tu tembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambayo ni kivutio namba moja cha utalii barani afrika. Ngorongoro utakutana na kivutio adhimu na akramu ambacho  ni  mchanga unaohama (Shifting Sand) unaoaminika  kwamba ndiyo sehemu pekee inayoweza warejesha watu ambao penzi lao limelegalega.

Mchanga unaohama ambao una umbo la nusu mwezi upo karibu na Bonde la Olduvai ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro. Mchanga huu wenye rangi nyeusi umetokana na madini ya chuma unatokana na majivu yaliyotokana na mlipuko wa Volcano kutoka Mlima Oldoinyo Lengai, mchanga huu ambao husogea kwa kasi ya takribani mita 15–29 kwa mwaka tuta lake lina urefu wa mita 5 na upana wa mita 100.

Watu walioishi maneo haya miaka mingi iliyopita walikuwa wakitumia mchanga huo ili kuweza kuunganisha upya mapenzi yao ama ndoa zilizotetereka husuluhishwa eneo hilo kwa watu kuomba na kutoa sadaka ya kutoa mikosi ama nuksi, hata wagumba hutumia eneo hili kuomba kupata watoto kwa kutoa Sadaka ambapo watu huzitumbukiza katika mchanga  huo na kuomba wanachokitaka.

Inaaminika kwamba mchanga huu unaohama ni mahsusi kwa kujenga mapenzi mapya kati ya wanandoa wawili au kama una mpenzi wako na unataka mapenzi yenu yawe ya kufa na kuzikana ukifika katika eneo hili na kugusa mchanga huu na kuomba basi hamuwezi kuachana na mwenza wako.

Eneo hili limepita umaarufu mkubwa na wageni wengi wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro kulitembelea  ili kuongeza nguvu ya mapenzi yao na kufanya waishi bila mikwaruzano.

Karibu Shifting sands katika Valentine hii hutojutia kuugusa mchanga huu na kulifanya penzi lako kuwa imara.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...