Farida Mangube, Morogoro
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro Sylver Rutagwelera, amefungua mafunzo ya awamu ya tatu ya Mfumo Jumuishi wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) kwa walipa kodi wa mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya matumizi ya mfumo huo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Rutagwelera amesema mfumo wa IDRAS umeleta maboresho makubwa katika utoaji wa huduma za kikodi kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo mawasiliano ya moja kwa moja kati ya walipa kodi na TRA, upatikanaji wa taarifa za kikodi pamoja na uwasilishaji wa huduma kwa njia rahisi na ya haraka.
Ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea walipa kodi uelewa sahihi wa matumizi ya mfumo wa IDRAS, kuongeza uwazi, ufanisi na usalama katika usimamizi wa kodi, sambamba na kujenga imani na kuhimiza ulipaji wa kodi kwa hiari.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka TRA Makao Makuu, Bi. Ernest Shirima amewahimiza walipa kodi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro kuuzoea mfumo mpya wa IDRAS akisema mfumo huo utatumika kusimamia na kukusanya kodi zote za ndani ya nchi kwa njia yenye ufanisi na urahisi kwa watumiaji.
Shirima amesema IDRAS ni mfumo unaokuja kuchukua nafasi ya mifumo mbalimbali inayotumika kwa sasa ndani ya TRA, na utaondoa matumizi ya mifumo ya karatasi (manual), hivyo kurahisisha usimamizi wa kodi za ndani kwa njia ya kielektroniki.
Ameongeza kuwa dhumuni kuu la kuanzishwa kwa IDRAS ni kuboresha huduma za usimamizi wa kodi za ndani, kuongeza ufanisi kwa walipa kodi na wadau wengine, pamoja na kupunguza matumizi ya mifumo mingi isiyounganishwa ambayo imekuwa ikileta usumbufu kwa watumiaji.
Naye Afisa Msimamizi wa Kodi wa Ofisi ya Mkoa wa Morogoro, Bwana John Magembe, amesema TRA imewawezesha walipa kodi kuufikia mfumo wa majaribio (Test System) ili waweze kujifunza na kuuzoea mfumo huo kabla ya kuzinduliwa rasmi. Amesema mfumo huo unapatikana katika kipindi cha mpito ili kuwapa watumiaji nafasi ya kufanya majaribio na kutoa mrejesho.
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mkoa wa Morogoro, Bwana Nickson Mugonya, amesema mfumo wa IDRAS unalenga kuimarisha utoaji wa huduma za kikodi kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na kutoa manufaa mbalimbali kwa walipa kodi na umma kwa ujumla, ikiwemo upatikanaji wa huduma kwa saa 24, utunzaji salama wa taarifa na kumbukumbu za kikodi, pamoja na ufuatiliaji wa maombi na usimamizi wa kodi kwa njia ya kidijitali.
Mafunzo ya matumizi ya mfumo wa IDRAS yanaendelea kutolewa kupitia njia mbalimbali, ikiwemo redio, televisheni na mitandao ya kijamii.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...