Dar es Salaam. Leo, Februari 9, 2026, Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Frederic Van de vyver Mkuu wa Jeune Afrique Media Group, kampuni inayoongoza ya habari ya ki-panafrika yenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, wamejadiliana ni kwa namna gani wanaweza wakafanya kazi pamoja katika fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.
Bw. Mchechu alimhakikishia Bw. De vyver kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba atapata ushirikiano wa kutosha.
“Kwa upande wa sekta ya umma utapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Hazin ana kwa upande wa sekta binafsi utapata ushirikiano kutoka kwa CEOrt,” alisema Bw. Mchechu.
Kwa upande wake Bw. De vyver alieleza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania.
“Lazima tutafute namna bora ya kushirikiana,” alisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...