Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewahimiza wananchi wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kuendelea kuitunza na kuilinda amani iliyopo, huku kikiwaonya kutokubali kushawishiwa kuivuruga kwa maslahi ya watu wasioitakia mema Tanzania.

Wito huo umetolewa leo ljumaa, Februari 20, 2026 na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Labani Kihongosi, alipokuwa akitembelea na kukagua uhai wa shina namba tano la Chama Cha  Mapinduzi katika eneo la Kasangezi, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Akizungumza na wanachama na wananchi wa eneo hilo, Kihongosi alirejea historia ya Mkoa wa Kigoma kuhifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani zinazokumbwa na machafuko, akisema hali hiyo inadhihirisha kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani kinachopaswa kulindwa kwa gharama zote.

"Msidanganywe na watu wanaotaka kuwalaghai mkaharibu amani ya hapa Kasulu. Hakuna shida kubwa kama kutangatanga katika nchi za watu. Msikubali kushawishiwa kufanya vurugu au mambo yatakayovuruga utulivu wenu. Lindeni amani ya hapa kwenu," amesema Kihongosi.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini na wanasiasa au watu wanaochochea vurugu, akidai kuwa mara nyingi wanaochochea migogoro hawaishi katika maeneo husika wala hawaguswi moja kwa moja na athari zake.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...