Mtendaji Mkuu Dkt. Maulid J. Maulid amefunga mafunzo ya uongozi na usimamizi wa shule yaliyoendeshwa kwa Wakuu wa Shule za Sekondari za Wilaya ya Arusha pamoja na viongozi wa elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Mafunzo hayo yameendeshwa na ADEM kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24-26 Februari, 2026 ADEM Bagamoyo.
Akifunga mafunzo hayo amewasisitiza viongozi hao wa elimu kwenda kuweka mkazo kwenye uongozi bunifu wa kimkakati unaoleta mabadiliko kama msingi wa maendeleo katika taasisi za elimu.
Pia amesisitiza juu ya uongozi jumuishi ambapo wanapaswa kushirikisha wadau, kusikiliza maoni ya jamii na kujenga mazingira ya uaminifu na uwajibikaji wa pamoja katika kufikia mafanikio ya usimamizi wa taasisi za elimu wanazozisimamia.
“Nawasihi mwende kuwa viongozi wenye maono, wenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kimkakati, na ujuzi wa kusimamia mabadiliko ya taasisi mnazosimamia kwa ufanisi kwani ninyi ndio mtachochea mabadiliko hayo”. Ameeleza Dkt. Maulid.
Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Elekezi Dkt. Lucas Mzelela amesema, mafunzo ya ADEM yamelenga kuwawezesha viongozi wa elimu kwa ujuzi wa vitendo, fikra za kimkakati na uwezo wa kusimamia taasisi za elimu kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko ya kweli katika sekta ya elimu.
Nae Mwenyekiti wa TAHOSSA Mkoa wa Arusha, Mwalimu Omari Nyangu ameipongeza ADEM kwa namna ilivyoendesha mafunzo hayo kwa umahiri na weledi mkubwa na kutanabaisha kuwa maendeleo ya sekta ya elimu hayawezi kupatikana bila uwekezaji katika kuwajengea uwezo viongozi na wasimamizi wa taasisi za elimu na mafunzo waliyopatiwa ni dira katika usimamizi wa taasisi za elimu wanazozisimamia.
Wakuu hao wa shule wamejengewa uwezo kuhusu utawala bora wa elimu, Mpango wa Jumla wa Maendeleo ya Shule, usimamizi wa utekelezaji wa Mtaala, ustawi na usalama wa wanafunzi shuleni, ushirikishwaji wa jamii katika kuleta maendeleo ya shule, usimamizi wa rasilimali za shule, kuzingatia itifaki na huduma kwa wateja pamoja na ufuatiliaji na tathmini wa shughuli za elimu shuleni.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...