Na Mwandishi Wetu, Tabora

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara,John Mongella, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, ameshiriki katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa mstaafu, Ndugu Nassor Hamdani.

Mazishi hayo yamefanyika leo Februari  3,2026 katika makaburi ya Mihogoni, Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora mkoani Tabora. 

Akizungumza katika ibada hiyo,Mongella amewasilisha salamu za rambirambi kutoka Chama Cha Mapinduzi, akimuelezea marehemu ndugu Nassor Hamdani kuwa alikuwa mshauri mwema wa Chama kwa kipindi chote cha uhai wake, sambamba na mchango wake mkubwa wa kujitolea kwa jamii.

Amesema CCM itaendelea kumkumbuka marehemu kwa uadilifu, hekima na mchango wake katika kukijenga Chama pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla.












 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...