Benki ya NMB imekabidhi vifaa mbalimbali katika shule za Msingi na Sekondari katika Mkoa wa Manyara kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji wa wanafunzi na ufundishaji ikiwa ni utaratibu wake wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii.
Mbali na sekta ya Elimu, Benki hiyo imekabidhi vifaa mbalimbali vya Afya kwenye Hospitali za Wilaya pamoja na Zahanati mbalimbali katika Mkoa huo, ambapo vifaa vyote vilivyotolewa katika sekta ya Elimu na Afya vimegharimu kiasi cha Sh Milioni 105.
Katika Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika jana Wilayani Hanang, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kaskazini Baraka Ladslaus alisema kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya shule na Hospitali katika Wilaya za Hanag, Mbulu pamoja na Babati.
Alisema kuwa NMB imetoa madawati 50 kwa ajili ya shule ya msingi Gidamambula, Vitanda 40 vya bweni (double decker) kwa ajili ya shule ya Sekondrai Katesh, huku Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini) ikipokea mabenchi 20 kwa ajili ya kupumzikia wagonjwa.
“ Mbali na hivyo vifaa NMB imekabidhi mabati 200 kwa Shule ya msingi Nanyemi, Shule ya msingi Mulbadaw nayo imepatiwa mabati 200, Shule ya Msingi Ng`abati imepata mabati 200, vifaa vyote hivyo thamani yake ni Sh Milioni 45” Alisema Ladslaus.
Aidha Meneja huyo wa Kanda aliongeza kuwa katika Wilaya ya Mbulu Benki hiyo imetoa viti 50 na meza 50 katika Shule ya Sekondari Kainam, Shule ya Msingi Kandach ikipatiwa madawati 50, Shule ya Sekondari Malang ikikabidhiwa viti 50 na meza 50.
Shule nyingine ni Sambaray shule ya Msingi ikikabidhiwa Madawati 50, Shule ya Msingi Giting ikikabidhiwa meza 10 na viti 10 kwa ajili ya walimu huku Hospitali ya Wilaya Mbulu ikikabidhiwa vitanda viwili vya kujifungulia wanawake wajawazito, vitanda 10 na magodoro 10 kwa ajili ya wagonjwa.
Alisema kuwa katika Wilaya hiyo vifaa hivyo vimegharimu Sh Milioni 22, ambapo katika Wilaya ya Babati Benki hiyo ilikabidhi Madawati 50 kwa shule ya Msingi Kiongozi huku shule za Msingi za Soraa na Singi zikipatiwa mabati 305 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa.
Aliogeza kuwa katika Wilaya hiyo Benki ya NMB imetoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za Afya katika Zahanati mbili, ambapo vifaa vyote vilivyotolewa katika Wilaya hiyo vimegharimu kiasi cha Sh Milioni 38.
Wakuu wa Wilaya za Hanang ,Mbulu na Babati waliipongeza Benki hiyo kwa kutoa vifaa mbali mbali vilivyogusa jamii moja kwa moja hususani katika sekta ya elimu na afya.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Almish Hazal alisema kuwa msaada huo unalenga kumaliza kero ya uhaba wa madawati kwa shule za Msingi amazo zimepata samani na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Michael Simindu alisema kuwa Wataedelea Kuiunga Mkono Benki hiyo kwa jinsi inavyojitoa kwa jamii katika kuboresha mazingira ya utolewaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika sekta ya Elimu na Afya.
Wanafunzi wa Shule mbali mbali za msingi na sekondari akiwemo Monica Allen wa Shule ya Msingi Sanubaray walishukuru NMB kwa kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika shule zao hali itakayochangia kuongeza kiwango cha ufaulu.

Mkuu wa wilaya ya Hanang Alimish Hazali (kulia) akikabidhiwa benchi na Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kaskazinid ,Ladislaus Baraka kwa ajili ya shule ya msingi Nantemi,Mulbadaw, N'gabati na Gidamambula zote za wilayani hapo NMB ilikabidhi mabenchi ,madawati,viti na meza na mabati kwa baadhi ya shule na hospitali za wilaya hiyo vyote vikiwa na thamani ya milioni 46.4 huku jumla ya misaada yote katika Mkoa wa Manyara ni sh milioni 105.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu ,Michael Semindu (kulia) akikabidhiwa madawati na Meneja wa Benki ya Nmb Kanda ya Kaskazini ,Ladislaus Baraka kwa ajili ya shule ya msingi Sanubaray ,Gidhim na Qandach zote za wilayani hapo ,NMB ilikabidhi mabenchi ,madawati,viti na meza na mabati kwa baadhi ya shule na hospitali za wilaya hiyo vyote vikiwa na thamani ya milioni 22.6. Jumla ya misaada yote katika Mkoa wa Manyara ni sh milioni 105.





.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...