Katibu wa NEC - Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ndg. Rabia Abdalla Hamid Februari 23, 2026 amekutana na makundi ya kijamii jijini Mwanza kwa dhumuni la kufuatilia maendeleo ya makundi hayo ikiwemo kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo.

Ndg. Rabia alieleza umuhimu wa uadilifu katika utumishi wa umma na kutaka uongozi wa serikali za mikoa nchini nzima, kutenga muda wa kusikiliza changamoto za makundi ya kijamii katika maeneo yao.

Aidha, ameielekeza serikali ya mkoa huo kufuatilia na kutekeleza, maagizo yakiwemo; gharama sahihi za leseni za madereva bodaboda, na suala la mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na mahitaji maalum. 

Pamoja na hayo alieleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kuendelea kuwapa kipaumbele makundi maalum  ikiwemo kupewa uwakilishi wa watu wenye ulemavu bungeni , bima ya afya kwa wote, kushiriki katika miradi ya ujenzi wa meli ya MV Mwanza, na ujenzi wa daraja la John Pombe Magufuli. 

Amemalizia kwa kusema kuwa serikali ya CCM itaendelea kuweka miundombinu muhimu katika kuwezesha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Mwanza na Tanzania nzima kwa kuwapa kipaumbele makundi maalum. Aidha, aliyaomba makundi hayo kuendelea kuiamini serikali ya CCM na kuiunga mkono.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...