Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dk.Samia Suluhu Hassan licha ya kukiri uwepo wa changamoto za kiusalama katika Bara la Afrika pia amepongeza jitihada mbalimbali zilizofanywa katika kukabiliana na migogoro.

Dk.Samia pia aligusia mchango uliotolewa na nchi ya Tanzania ambayo ni mchangiaji wa hali na mali pamoja na vijana wake katika kulinda amani barani Afrika.

Akizungumza Ikulu Dar es Salaam alipokuwa akielezea yaliyojiri katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema pia katika miaka minne ujumbe wake Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika Baraza Kuu la Usalama na Amani la AU ulihusu masuala yanayosimamiwa na Baraza  ikiwemo uchaguzi, pia Amani na usalama.

“Wakati wa Baraza hilo la Usalama na Amani la AU Rais Dk.samia Suluhu Hassan pia alieleza changamoto zilizotokezea nchini kwake na kuelezea pia jitihada za Serikali yake bila kuhitaji msaada kutoka nje zilizofanywa na Serikali yake kukabiliana na changamoto hizo zilizotokea

“Sisi tunaweza kuona changamoto zetu kubwa sana lakini kule ni kama punje tu ya ngano kwasababu ukichukulia migogoro ya wenzetu ni mikubwa zaidi ,ni mipana zaidi ya miaka mingi,huku kwetu ni kama upepo unaopita,”amesema Waziri Kombo 

Wakati anaeleza hayo Waziri Kombo amesema kwamba “Kama mnavyojua Tanzania imekuwa ni Mjumbe katika Baraza la Usalama na Amani la AU kwa miaka minne mfululizo mara mbili na mwaka 2029 Mungu akijaalia Tanzania itakuwa mjumbe katika Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Mataifa.

Ambapo amesema kwa hivi sasa Tanzania ilianza tokea mwaka 2022 hadi mwaka huu wanapomaliza rasmi kuwa mjumbe wa baraza la usalama na amani Barani Afrika.

“Na ndio  maana sisi ushiriki wetu ulikuwa mkubwa wakati wa vikao vya Baraza hilo la Usalama na Amani kuanzia  mwanzo kwenye ajenda mpaka uwasilishaji kwenye Baraza Kuu.”

Akieleza zaidi pia amesema katika  mkutano wa AU ajenda Kuu ilikuwa hali ya usalama na amani barani Afrika ambapo Waziri Kombo amejulisha kwamba waheshimiwa wakuu wa nchi zote walijikita kujadili ajenda hiyo kwasababu hali ya usalama na amani sio shwari barani Afrika

“Afrika tunapitia  wimbi la mtihani ambalo linatokana na mambo mbalimbali yakiwemo ushindani wa rasilimali zilizokuwepo barani Afrika ambalo kwa sasa linaonekana kwa duniani ndio limebakia kuwa na rasilimali nyingi zaidi kuliko bara lolote lie duniani na hii ni kwa takwimu na kisayani 

“Kwa lugha nyingine utajiri mkubwa uko barani Afrika zaidi kuliko bara lolote,ukichukua utajiri wa maji,rotuba ndani ya aridhi,utajiri wa hali ya hewa ,utajiri wa oksijeni tunayovuta duniani. Kwahiyo utajiri wa kıla aina ,pamoja na afya,mazingira na rasilimali nyingine ikiwemo madini zimekuwa visababishi vya uwepo wa migororo tunayoina kwa nchi za Afrika.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...