Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Februari 27,2026 ameandaa Iftar maalum kwa wakazi wa Mkoa huo hafla ambayo imefanyika katika ukimbi wa Diamond Jubilee.Katika hafla hiyo viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam wamehudhuria.
Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mufti Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakar Zubeir bin Ally ambaye aliwaongoza waumini katika dua ya kuiombea nchi amani, mshikamano na maendeleo endelevu.
Akizungumza katika hafla hiyo RC Chalamila aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kuendeleza umoja na upendo miongoni mwao, akisistiza kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kusaidiana. Alieleza Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Viongozi wa Dini katika kudumisha amani na utulivu.
Kwa upande wa Mufti Mkuu aliishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuandaa Iftar hiyo, akieleza kuwa matukio ya aina hiyo huimarisha uhusiano kati ya Serikali na Jamii ambapo ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuiombea nchi na kuzingatia maadili katika kipindi hiki cha Ramadhani.
Hafla hiyo ilihitimishwa kwa futari ya pamoja iliyoambatana na mawaidha mafupi ya kidini huku washiriki wakionyesha furaha na mshikamano mkubwa.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...